Maji ya matunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Bilauri ya sharubati ya machungwa.

Maji ya matunda (pia: juisi kwa neno la mkopo kutoka Kiingereza "juice"; au: Sharubati kwa neno lenye asili ya Kiarabu) ni kinywaji kinachotokana na matunda ya mimea na kinachotengenezwa kwa kusindika tu matunda ya aina moja au mchanganyiko wa matunda mengi.

Kuna aina nyingi sana za sharubati, sawa na wingi wa matunda yanayolika. Hasa matunda yenye majimaji mengi ndani yake yanafaa kwa kuyatengeneza.

Watu wengi hupenda kunywa sharubati, kwa mfano ya

na mengine mengi.

Pamoja na utamu wake, kinywaji kama hicho kinafaa sana kwa afya, kwa sababu kinaongeza haraka vitamini muhimu mwilini.

Kama tunda lina asidi nyingi kiasi ndani yake sukari huongezwa, lakini matunda mengine, hasa kama ni mabivu na yameiva penye jua kali, huwa na sukari ya kutosha ndani yake.

Katika nchi nyingi maji ya matunda hutengenezwa kiwandani na kuuzwa madukani. Watu wengi wanajua na wanapenda zaidi kujitengenezea nyumbani.

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maji ya matunda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.