Majadiliano ya mtumiaji:Siwema Nikini

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:09, 9 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Picha ya Joanne Grants[hariri chanzo]

Salamu katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Joanne_Grant umeweka picha ambayo siyo yenyewe, tafadhali angalia sana picha unazoweka zisije kuleta uharibifu katika makala, na picha ambazo hazina mahusiano na makala hazifai kubandikwa katika makala husika, pitia makala yako,Amani sana Idd ninga (majadiliano)

Dada, naona unafutafuta "mwaka" na "mnamo", kumbe Kiswahili kinapenda maneno hayo, tofauti na Kiingereza. Tafadhali, usiendelee. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:56, 14 Machi 2022 (UTC)[jibu]

Masahihisho ya kurasa mpya zilizo undwa tarehe 17.09.2022[hariri chanzo]

Ndugu Siwema Nikini Salam, Nakuandikia ujumbe huu kukujulisha kuwa unaimbwa ufanyie marekebisho kwenye makala zako tajwa hapo juu. bila kufanya hivo utafungiwa kuhariri kwa muda. Mambo ya kuzingatia 1. fomati ya makala 2. interwiki 3. Vyanzo 4. Jamii 5. Tafsiri ya kompyuta 6. en haiwezi kutumika kama chanzo 7. viungo vya ndani 8. Marejeo au tanbihi 9. makosa ya tafsiri na misamiati ya sayansi

-- Olimasy (majadiliano) Olimasy (majadiliano) 07:28, 17 Septemba 2022 (UTC)[jibu]

Sawa nafanyia kazi Siwema Nikini (majadiliano) 03:28, 18 Septemba 2022 (UTC)[jibu]
Hongera, naona maendeleo yako. Usisahau kuunganisha makala zako na lugha nyingine upande wa kushoto. Asante na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:13, 18 Septemba 2022 (UTC)[jibu]

Habari, baada ya kuona mchango huu napaswa kuipendekeza kwa ufutaji. Kwanza unaleta makala ambayo haieleweki kwa nini mwimbaji huyu atajwe katika wikipedia (hujatafsiri habari yoyote inayoeleza umuhimu au umaarufu wa mtu huyu), pili umejaribu kusahihisha tafsiri ya kompyuta lakini kwa namna isiyoeleweka kabisa. Matokeo haikubaliki. Je muziki mbadala ni kitu gani?? "uingereza Colombia" ni kitu gani?? Tena "Marekani-Kanada" ni nchi gani?? Najua unachojaribu kusema maana nimeangalia makala ya enwiki (hapo umesahau kuweka interwiki) lakini tokeo haifai kuwepo katika wikipedia hii. Ukipenda usaidizi, tafadhali niandikie email kupitia "Email this user" (utaiona kwenye menyu ya ukurasa wangu). Lakini naomba usilete tena kazi ya namna hii. Kipala (majadiliano) 23:07, 9 Aprili 2023 (UTC)[jibu]

sawa ngoja niifute Siwema Nikini (majadiliano) 05:46, 10 Aprili 2023 (UTC)[jibu]
Asante ila naomba uangalie majaribio yako kwa jumla. Nikipitilia naona udhaifu : 1) mara nyingi ulitafsiri mstari wa kwanza wa makala ya Kiingereza tu.mKutoka sentensi hii haionekani kwa nini mtu yule awe na makala katika wikipedia yetu, yaani hakuna umaarufu au umuhimu wowote uanoonekana.(mfano makala 19-23 na mengine) 2) mara nyingi unajaribu kutafsiri neno-kwa-neno na matokeo yake ama hayaeleweki au hayaleti maana. Kutafsiri ni kushika maana ya habari na kuieleza kwa maneno yako yanayoeleweka. 3) Unajaribu kutafsiri pia mada ambako unakosa msamiati, mfano "climate justice" (si haki ya hali ya hewa!), "Hali ya hewa ya Apocalypse", na mengine.
Nikushauri utafute mada unayoelewa, jaribu kutafsiri hadi unadhani umeweza kueleza ujumbe, halafu uulize wahariri wenye uzoefu wanaonaje. Kama ni watu, angalia orodha hiyo: List Category Tanzanian people en ambako utakuta makala kuhusu watu wa Tanzania katika wikipedia ya Kiingereza ambazo hazikutafsiriwa bado kama zinaonekana kwa rangi nyekundu. Kipala (majadiliano) 17:48, 10 Aprili 2023 (UTC)[jibu]
sawa nitafanya marekebisho Siwema Nikini (majadiliano) 14:44, 11 Aprili 2023 (UTC)[jibu]
Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

(mifano Anna Rose, Alan Hastings) Kipala (majadiliano) 16:28, 28 Juni 2023 (UTC)[jibu]