Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Praygod mwanga

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Habari, asante kwa michango. Tafadhali usisahau kuunganisha makala unayoanzisha kwenye Wikipedia:Jamii na pia interwiki.

Hello,

I need help to improve the article Salzburg please. I am learning Kiswahili right now, but I am in a starter level, I can not do it on my own Bro. Could we work together? I know Salzburg very good, but I need help in Kiswahili language. What about if I write some more text into the article and you check and correct my Kiswahili language?

Kind regards,

Alex 84.174.183.93 03:33, 28 Novemba 2020 (UTC)[jibu]

Can you help me correct an article? Thank you!

[hariri chanzo]

Hello, @Praygod mwanga:! I wrote an article on Andrea Benetti, a well-known Italian artist https://en.wikipedia.org/wiki/Andrea_Benetti_(artist). I used the automatic translator to make a draft https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:BarbaraLuciano13 . Could you help me correct the text and add the infobox with the photo at the beginning and the categories at the bottom? Unfortunately I don't know the language and I am not able to do it ... Thanks for what you can do, see you soon, --BarbaraLuciano13 (majadiliano) 09:11, 19 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Nimekusimamisha kwa kutumia google-translate bila kuisaisha

[hariri chanzo]

Habari zako, nimepitilia makala ya VVU / UKIMWI nchini Jamaika. Hapa umemwaga matini ya google-translate kwa asilimia zaidi ya 99. Desturi hii imeleta makala ambazo zina lugha mbaya isioeleweka. Ingawa sehemu uliyotafsiri ilikuwa fupi (na hivyo inawezekana kuhisi maana yake nini) ni mfano mbaya. Wewe umefahamishwa hapo juu (sanduku la "Karibu") kwamba ni mwiko kumwaga matini ya google translate. Umepuuza utaratibu huu. Ninakuzuia sasa. Unaombwa kuwasiliana nami (kwenye ukurasa wangu wa majadiliano au kwa kuniandikia email (bofya "Email this user" kwenye ukurasa wangu, utaiona upande wa kushoto) na ueleza lini na jinsi gani utasafisha kurasa zako. Kipala (majadiliano) 08:26, 12 Agosti 2021 (UTC)[jibu]


Praygod mwanga (majadiliano)habari Kipala,mbona mimi sijaandika hiyo makala, nimeeandika moja tu ya bandari ya mtwaraPraygod mwanga (majadiliano)

Samahani, nimeshaondoa zuio. Niliitambua sasa hivi! Nimewachanganya. Kazi njema! Kipala (majadiliano) 08:47, 12 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Matumizi ya google translate

[hariri chanzo]

Ndugu nimepitilia Bandari ya Tanga naona unatumia google translate ukijaribu kuisahihisha. Tafadhali uwe makini zaidi! Sentensi kama hii "Kwa sasa, bandari hii inahudumiwa na kampuni tatu shipping lines" haifai. Pia ukipitilia harakahaaka tu unapata sehemu kama "kutoka Uganda kwenda Kenya hadi bandari ya Lamu Kusini mwa Sudan na Ethiopia" ambayo haina maana kwa sababu Lamu si kusini mwa Sudan, ulijaribu kufupisha google translate bila kuisoma vema. Tatizo la google translate ni (hata ukisahihisha) kwamba unafuata muundo wa matini ya Kiingereza ambayo mara nyingi haifai kama sentensi za Kiingereza ni ndefu; tokeo lake si Kiswahili.

Mara kwa mara ni lazima kutuma lugha yako badala ya kwenda neno-kwa-neno na kufuata google. Pia ni lazima kutafakari kabla ya uchukua matini ya enwiki. Makala kuhusu Bandari ya Bagamoyo ni bure; sio wewe unaishi Tanzania? Hujui kwamba habari za makala ya enwiki si kweli? Magufuli alibatilisha mapatano yote baada ya 2018 (tarehe ya makala ile) na sasa kuna tangazo kwamba labda majadiliano yanaanza tena. Ama usahihishe makala au tuifute kabisa maana habari si kweli. Kipala (majadiliano) 10:05, 12 Agosti 2021 (UTC)```[jibu]

```Sawa nitairekebisha```

Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:28, 19 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Nakubali kwa furaha ombi lako la kuondolewa zuio, nikitarajia utaendelea kwa bidii kutunga na kuhariri makala, ila kwa umakinifu zaidi, bila ya kuamini tafsiri za Google: kwa jumla hazieleweki. Afadhali makala fupi nzuri kuliko ndefu zinazochafua Kiswahili na Wikipediua yetu. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:46, 20 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Herufi koze si fomati ya kawaida

[hariri chanzo]

Ndugu nilifuta masahihisho yako kwenye makala Nuhu Abdullahi. Uliingiza mara nyingi herufi koze bila kujali mwongozo wetu wa staili. Angalia Wikipedia:Mwongozo_(Muundo). Kipala (majadiliano) 14:53, 18 Septemba 2021 (UTC)[jibu]

Lugha za Kiafrika

[hariri chanzo]

Ndugu, unaendelea kutunga kurasa ambazo zipo tayari. Hasa lugha nyingi zimeshaanzishiwa makala na Baba Tabitha. Afadhali ushughulikie mambo mengine, k. mf. miji. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:33, 20 Machi 2024 (UTC)[jibu]

Asante Praygod mwanga (majadiliano) 10:43, 20 Machi 2024 (UTC)[jibu]
Pia unajua kwamba kwa Kiswahili lugha ya Chagga tunaiita Kichagga na watu wa Chagga tunawaita Wachagga. Ni vilevile kwa Akan, Yoruba n.k. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:41, 23 Machi 2024 (UTC)[jibu]
Asante kwa kunielekeza nimejifunza nitafanya masahihisho. Praygod mwanga (majadiliano) 08:08, 23 Machi 2024 (UTC)[jibu]
Mbona umeongeza lugha ya Kamba? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:33, 30 Machi 2024 (UTC)[jibu]

Futiboli ya Marekani

[hariri chanzo]

Ndugu, hongera kwa kufululiza kutunga makala juu ya wachezaji wa Marekani. Ila ungefanya vizuri kuweka wazi kuwa mpira wa miguu wanaoucheza si soka bali futiboli ya Marekani ambayo ni tofauti sana. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:11, 22 Septemba 2024 (UTC)[jibu]

Ndugu, hongera kwa maendeleo yako makubwa. Kwa kawaida sasa sihitaji kurekebisha kurasa zako. Lakini naomba ujitahidi kuunganisha hizi za Kiswahili na zile za lugha nyingine. Fungua "zana" juu kulia, bonyeza "Hariri viungo vya lugha zingine", litatokea sanduku ambamo upande wa juu uandike "en" na chini jina la ukurasa kama wa kwako kwa Kiingereza. Asante kwa ushirikiano na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:27, 30 Septemba 2024 (UTC)[jibu]

Kupitia masahihisho

[hariri chanzo]

Ndugu, hongera kwa juhudi zako. Maendeleo yapo, ila naomba upitie mabadiliko ya makala zako kwa sababu unarudiarudia makosa yaleyale nami nalazimika kurudiarudia masahihisho yaleyale. Ningekuwa na muda zaidi ningeboresha zaidi lakini naishia kufanya yaliyo muhimu zaidi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:04, 17 Oktoba 2024 (UTC)[jibu]

Asante na Samahani nitajitahidi kuwa mwangalifu zaidii Praygod mwanga (majadiliano) 19:16, 17 Oktoba 2024 (UTC)[jibu]
Naomba unieleweshe zaidi ni wapi ninapo kosea ili niweze kujirekebisha vizuri Asante. Praygod mwanga (majadiliano) 20:06, 17 Oktoba 2024 (UTC)[jibu]
Habari ndugu @Praygod mwanga nakupongeza kwa kuendelea kuhariri , nakukumbusha kuweka viungo vya ndani (internal link ) katika makala zako. ni nyema kufwatilia masahihisho ya makala zako ili ujue ni wapi pakurekebisha. Amani kwako Justine Msechu (majadiliano) 09:09, 23 Novemba 2024 (UTC)[jibu]
Kweli umepiga hatua! Ila uelewe kigezo {{BD}}. Ni hivi: {{BD|Mwaka wa kuzaliwa, yaani, 1958|usiweke kitu - ila kama mtu kafa weka mwaka aliokufa, yaani, 2009}}

Chumba cha kwanza mwaka wa kuzaliwa tu Chumba cha pili mwaka aliokufa ANGALIZO Usiweke jamii yoyote kama vile: "waliozaliwa", "waliofariki", na "watu walio hai". Ukiweka {{BD|1950|}} - katika jamii itataja "waliozaliwa 1950" na "watu walio hai". {{BD|1950|2012}} - katika jamii itataja "waliozaliwa 1950" na "waliofariki 2012". Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:30, 5 Desemba 2024 (UTC)[jibu]

Nashukuru sana kwa kuendelea kunielewesha natamani kupiga hatua zaidi. Praygod mwanga (majadiliano) 12:19, 5 Desemba 2024 (UTC)[jibu]
Ndugu samahani nimekutana na changamoto hii mwaka wakuzaliwa upo ila mwaka wakufariki haujulikani na nikiandika hivi katika jamii itasema waliozaliwa 1897 na watu walio hai nafanyaje iweze kuwa katika Jamii waliozaliwa 1897 na mwaka wakufariki haujulikani samahani kwa usumbufu naomba unisaidie katika hili. Praygod mwanga (majadiliano) 11:07, 6 Desemba 2024 (UTC)[jibu]
Unaweza kuandika {{BD|1897|mwaka usiojulikana}}. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:21, 6 Desemba 2024 (UTC)[jibu]
Nashukuru sana Praygod mwanga (majadiliano) 06:42, 7 Desemba 2024 (UTC)[jibu]
Nimeandika hivi {{BD|1897|mwaka usiojulikana}} lakini kwenye Jamii inaleta mwaka usiojulikana kwa maandishi yenye rangi nyekundu ni sawa au nitakuwa nimekosea wapi samahani kwa usumbufu. Praygod mwanga (majadiliano) 06:55, 7 Desemba 2024 (UTC)[jibu]
Ni sahihi kwa sababu hatujaanzisha jamii hiyo. Nitafanya hivyo mapema. Aamani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:58, 7 Desemba 2024 (UTC)[jibu]