Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Msafiri

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Mwanaharakati (majadiliano) 13:26, 2 Agosti 2008 (UTC) Ok nimeona maneno yako ya mwanzo huko ila sijui uliona makala zangu zote nilizoandika katika Wikipedia ya kiswahili, maana usitizamii hii ya Ballack ya Ballack hiyo uliyoona hapo niliandika tu haraka haraka kama unataka uone makala nzuri ambazo nilizoandika tafuta Mohamed Zidan,Dugary,Saidi Ntibazonkiza na Valery Nahayo nakuna nyingi tu nategemea hata upangiliaji wangu ulitoka mzuri zaidi kwani baada naona ulipasishwa moja kwa moja. Unajua ujumbe ambao umenifikishia ndugu yangu kwa siwezi kukasirika kwani duniani watu kama wewe ni wengi sana ambao kusahihisha wenzio kwa njia kama hii unayotumia wewe uliona makala moja ukafikiri ndio zote. Ndugu yangu mimi siwezi acha toa mchango wa aina yoyote katika Wikipedia ya Kiswahili kwani hii inahusu watu wanaozungumza Kiswahili toka nchi maarufu zinazozungumza Kiswahili. Sina mengi ila nakutakia mafaanikio mengi katika kila jambo[jibu]


Msafiri, salam! Nimeona makala zako nyingi zenye kuhusiana na maswala ya mpira, lakini pia nyingi zimekosa mpangilio mzuri na vitu muhimu katika makala. Na ndiyomaana ulivyoanza kuandika kuhusu mpira, mie nikaanza kuumba template ya mchezaji ili uweze kurahisisha kazi zako! Lakini bado naona mara nyingi zilizokosa kitu kama "Jamii" (Category), kitu ambacho ni muhimu sana katika kutaja makala na wachezaji nchi kwa nchi na hata miaka kwa miaka. Basi JAMII hurahisisha kazi ya kutafuta makala zenye kufanana!! Labda ungeangalia makala ya Ronaldinho, huenda ukapata fikra mbili tatu pia kama utapenda kutembelea zile makala za awali, yaani ulizozianzisha halafu mie nikaziweka sawa na hata kuziwekea jamii. Basi usijisikie vibaya kwa vile nimesema hivyo ndiyo ukakasirika, la. Nataka tuwe tunasaidiana kuwekana sawa katika mswala fulanifulani! Nikiwa natokea Dar es Salaam, Tanzania, niite Muddyb Blast au--Mwanaharakati (majadiliano) 05:25, 18 Agosti 2008 (UTC)[jibu]

Ni furaha iliyoje kumpata mtu mwenyekusomea Kiswahili hiki katika Chuo Kikuu. Labda tu nikupe pongezi juu ya uchangiaji wako, lakini pia usisite kuulizwa swali lolote ujisikialo!!! Kwani tupo kwa ajili yako. Karibu sana mwanaharakati wa "Kandanda".--Mwanaharakati (majadiliano) 16:29, 18 Agosti 2008 (UTC)[jibu]


Ok nimeona maneno yako ya mwanzo huko ila sijui uliona makala zangu zote nilizoandika katika Wikipedia ya kiswahili, maana usitizamii hii ya Ballack ya Ballack hiyo uliyoona hapo niliandika tu haraka haraka kama unataka uone makala nzuri ambazo nilizoandika tafuta Mohamed Zidan,Dugary,Saidi Ntibazonkiza na Valery Nahayo nakuna nyingi tu nategemea hata upangiliaji wangu ulitoka mzuri zaidi kwani baada naona ulipasishwa moja kwa moja.

Unajua ujumbe ambao umenifikishia ndugu yangu kwa siwezi kukasirika kwani duniani watu kama wewe ni wengi sana ambao kusahihisha wenzio kwa njia kama hii unayotumia wewe uliona makala moja ukafikiri ndio zote. Ndugu yangu mimi siwezi acha toa mchango wa aina yoyote katika Wikipedia ya Kiswahili kwani hii inahusu watu wanaozungumza Kiswahili toka nchi maarufu zinazozungumza Kiswahili. Sina mengi ila nakutakia mafaanikio mengi katika kila jambo

Salam. Ndugu Msafiri, sikusema vile kwa ubaya, la. Nilikuwa najaribu kuweka mambo sawa! Halafu kumbuka kila makala utakayoandika, basi ujue mie lazima nitaiona tu! Na kama unakumbukumbu mie ndiyo niliyoongeza kitu kama "Template:Infobox football player" kwa ajili ya kukupa motisha katika swala zima la ujenzi wa makala zako za mpira! Sidhani kama nimefanya baya lolote la kukupelekea kuwa hivyo. Si kitu. Je ulipitia tena zile makala zako na kuongezea kitu kama JAMII? Ni muhimu sana kuweka CATEGORY katika kila makala uziumbapo vinginevyo zitakuwa hazina kumbukumbu rasmi! Mengineyo: Nimeona ukiacha ujumbe wako bila ya kutia sahihi yako. Unashauriwa baada ya kumaliza kuandika ujumbe wako, uuandike alama hizi --~~~~. Hizo zitaweka jina lako zenyewe na tarehe ulioandika ikiambatana na muda! Kazi njema na kila lakheri!!--Mwanaharakati (majadiliano) 06:08, 20 Agosti 2008 (UTC)[jibu]

Mohamed Zidan

[hariri chanzo]

Salaaam! Nimefanya masahihisho kadhaa katika makala ya Mohamed Zidan. Ukiangalia utano nimeweka kitu kama VICHWA VYA HABARI, JAMII AU CATEGORY, VIUNGO VYA NJE, NA INTERWIKI, yaani kama makala inawezekana kupatikana kwa lugha nyingine, basi InterWiki ni muhimu pia! Utaona nimeongeza orodha ya baadhi ya Klabu kwa kutumia mfumo wa jedwali la template. Pia nimewekea ile kitu inayoitwa "PARAGRAPHY" katika maeneo muhimu. Natumai tupo pamoja kwa kila hatua tuendapo! Mengineyo: Unatakiwa ufuate ule wa makala hiyo ya Mohamed Zidan, ndiyo ujenge makala zingine, makala inaulazima sana wa kuwekewa CATEGORY NA INTERWIKI, ikiwezekana hata VIUNGO VYA NJE!! Natumai umepata Nd. Msafiri. Basi kila lakheri na usisahau kuwasalimia huko Misri ulipo!--Mwanaharakati (majadiliano) 16:09, 20 Agosti 2008 (UTC)[jibu]

Salaam kwa kweli nimeona mambo fulani muhimu ambayo kabisa mimi nilikua siweki ila umenisaidia kabisa kuyaunda kweli unahaki katika kunisaidia ila barua yako ya mwanzo kabisa ilikuja kali kabisa kutokana na usahihishaji wako ila kwa kweli nakumbuka kuna makali niliwai kuunda ya Dugary mimi kuja siku ya kufatia nikakuta umeniweka mambo yakuhusu (category) na viungo vingine muhimu na mimi nikafika napatia njia katika kuweka katika makala ya Valery na Saidi. Mimi sikataa kabisa kupata msaa kwako tena nitashukuru sana maana hapa sote nikutumika kwaajili ya Lugha ya Kiswahili. Ok nakushukuru sana hata barua zako zilizofata kwa kweli umeziandika vizuri zaidi. Msafiri

Basi sawa. Karibu sana na usijali kuhusu yaliyopita! Kwani sisi sote ni wachangiaji tu, na wala hakuna haja ya kulaumiana kwa lolote lile. Karibu tena.--Mwanaharakati (majadiliano) 07:35, 23 Agosti 2008 (UTC)[jibu]

Vipi ndugu yangu ninafurahishwa sana kutokana na mchango ambao unanisaidia katika baadhi ya makala hua naweka hapa kwenye Wikipedia hata hiyo makala ya mchezaji kutoka Tanzania naona umenisaidia,kwa zamani nilikua na muda ila hizi siku tokana na masomo ya nje ambayo ninayosoma hua ndio nikiingia net naona niache hata makali moja kwa wiki. Nakutakia kila la kheri naninahisi uko mtu mzuri. Msafiri

Basi karibu tena!! Na tutaendelea kusaidiana kila siku ziendapo!!! Kila lakheri,--Mwanaharakati (majadiliano) 13:54, 28 Agosti 2008 (UTC)[jibu]

Hongera!

[hariri chanzo]

Msafiri, salaam! Hongera kwa makala ya Dennis Oliech. Umeifanya vizuri kuliko zote za awali. Nafurahia kuona unazidi kukua katika ujenzi wako wa makala za wachezaji wa mpira wa miguu! Ukiangalia pale utaona nimeongoza picha tu na masahihisho madooogo kabisa. Lakini pongezi kubwa linakuja kwako wewe bwana Msafiri! Haya, labda ningekuongezea mawili-matatu ambayo baadaye yatakusaidia katika kuweka picha za wachezaji wako wa mpira. Fuata taratibu hizi:

1. Ukiwa unaenda katika Wikipedia kwa Kiingereza utaona maandishi yameandikwa hivi:

    • image =[[Image:Dennis Oliech.jpg|250px]]

Wewe chukua kuanzia hapa:

    • [[Image:Dennis Oliech.jpg|250px]] (kwa matumizi ya baadaye na sio mchezaji huyu).

Kisha njoo katika Wikipedia ya Kiswahili, halafu paste baada ya kukopi hayo maelezo.

2. Utaona mimi nimemwekea mwaka wa kuzaliwa katika jedwali la mchezaji huyo, yaani yenyewe inataja ana umri gani (umri ndani ya mabano). Nalo unachukua kama lilivyo kutoka Wikipedia kwa Kiingereza! Soma maandishi haya:

    • {{birth date and age|1985|2|2}}

Sasa wewe unatakiwa uongeze hiki | baada ya 2 au namba ya mwisho! Kisha unaandika neno:

    • df=yes

Basi yenyewe itasema mwaka aliozaliwa ikiwa pamoja na umri wake!! Mimi nakutakia kila lakheri katika maisha yako na kukutakiwa furaha ya michango ya Wikipedia yetu tukufu. Niite Muddyb Blast au,--Mwanaharakati (Longa) 17:19, 17 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]

Muheshimiwa Muddyb Blast kwanza nakutakia siku njema nakwakunizidishia mambo mengi kabisa mimi bila kukuficha ninakushukuru sana kwakunisaidia mimi ni Mrundi ila ni mtu ambae ninapenda sana Kiswahili naninapenda nitoe michango aina mbali mbali katika vitu vinavyo husu kiswahili kweli namna yakuweka Categories nilikua sijui ila wewe ndio umenisaidia yaani upangiliaji kwa ujumla,mimi nitakua tayari katika kushiriki katika hii Wikipedia yetu ya Kiswahili na hili swala la picha ndio hata juzi nilitaka kukuandikia nikuulize namna yakuweka picha lakini nimeona nakujua, nilikua nataka unielekeze namna yakuweka picha mpya ambayo haijawekwa kwenye Wikipedia nitaweka aje?. Usiwi na shaka mimi nimesoma mengi kwako nanitajitahidi kuvitumia na yote hayo tunatumika kwaajili ya faida ya Lugha ya Kiswahili naitakua vyepesi kwangu maana nina komputa ndani. Ama jambo lingine mimi ni mwanariadha ambae nafatilia sport kwa wingi sana hilo ni swala nitakua karibu nalo na namna umenipa mwanga nahisi wepesi kufanya kazi yangu bila kiziwizi na jambo lolote litakua linanisumbua nitakua nakuuliza wangu nakushukuru sana. Maisha mema na kazi njema.

Masafiri, salam. Kuhusu picha, waweza kupakia kwa kutumia hapa. Lakini hizo picha zinakuwa na matatizo ya hatimiliki. Je, wewe hizo picha ni zako? Au umepiga wewe mwenyewe?--Mwanaharakati (Longa) 13:12, 18 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]

Bwana habari za siku ndugu yangu. Nimeona mabadiliko kidogo ambayo uliyoweka katika makala nilizofanya nikaona nikuandikie nakutoa shukurani kwa mchango huo kwani mambo ninayotumia ni msaada kutoka kwako. Ninakushukuru sana kwa hilo. Vipi ndugu yangu habari za siku, ningeliandika mengi ila tu niko katika maandalizi ya mitihani nakutakia mafaanikio mema katika kila jambo.

Nawe pia! Lakini hapa nina swali moja: Kwani wachezaji mpira wa Burundi wana uwezo wa kuichezea timu ya taifa ya Rwanda?--Mwanaharakati (Longa) 05:43, 27 Novemba 2008 (UTC)[jibu]

Asante sana kwa swali lako Burundi wanazungumza Kirundi na Rwanda wanazungumza Kinyarwanda lakini ilikua inastahili iwe lugha moja maana wote wanafahamiana nakuzungumza vizuri,Ligi kuu ya Rwanda wachezaji wa kirundi ni wengi sana wanaocheza huko sasa wakionekana wachezaji wazuri wanafika wanawapa pesa ili wachezee timu ya taifa na timu ya Taifa ya Rwanda na hao wanakua hawajawai kuchezea timu ya taifa ya Burundi katika mechi za kimataifa kwani ni marufuku mchezaji wa nchi fulani kama alishacheza mechi za kimataifa achezee timu nyingine ila tu kama atakua amechezea timu za vijana na mwisho timu ya myaka 20 kama vile Kanoute na Sisoko hao wamezaliwa Ufaransa wakachezea huko na timu ya ya Taifa ya Ufaransa ya vijana,ndio kanuni ya Fifa,kama kijana Kassim Bizimana ni mchezaji kutoka Burundi kazaliwa Burundi familia pia lakini Rwanda ilituma watu kuweza kumuomba achezee timu ya Rwanda lakini alikataa akasema mimi nitachezea timu ya Burundi na hiyo ilikua mwaka mwaka 2007,lakini Rwanda sio hivyo tu ila imefikia kuwapa uraia wachezaji kutoka Kongo na kisiwa kimoja huko kinaitwa(Guadeloupe)http://en.wikipedia.org/wiki/Fritz_Emeran wala hajui Kinyarwanda,lakini sio Rwanda tu ni nchi nyingi hadi ulaya na nchi za ghuba kama Katari Imarati na zingine mpira kwa sasa umekua ni biashara kwani pesa zinawekwa mbele kuliko mpira kwa sasa Robinho ameenda Manchester City nakukataa Chelsea kutokana na mshahara na pesa zakununuliwa. Nategemea utanifahamu,na ndio maana unaona mpira wa Rwanda unakua kwa kasi kwani wanatumia pesa zaidi hata katika ligi yao au timu yao ya taifa nategemea Rwanda hawashindi Mpira Kenya au Uganda nategemea hata Tanzania lakini namna najua wanatumia pesa. Serikali ya Burundi hua haitowi pesa au kuleta wachezaji wao wanaocheza Ulaya tena wanaocheza kwenye klabu kubwa kubwa baadhi kama Shabani Nonda hivi anachezea(Kongo) Mungine anacheza Spain katika klabu nzuri anaitwa Muhammad Tchite (Recing Santader) alichezea timu ya taifa ya Burundi ya vijana ya myaka 20 lakini alipita Rwanda kwa myaka miwili hivi Ubelgiji imempa uraia ili achezee timu ya taifa lakini Fifa iliwakatalia nakusema kua alishachezea timu ya Burundi ya vijana nitakupa sababu karibuni, yaani timu hiyo ya Taifa ya Burundi inaweza kua na timu kuanzia goli mpaka mshambuliaji kutoka ulaya. Nakutakia kila la kheri.

Muundo wa mwaka na tarehe za kuzaliwa

[hariri chanzo]

Msafiri, salaaam! Kwanza kheri ya mwaka mpya. Pili nina haya ya kukueleza: Nimeona mara nyingi ukiandika jina la Mhusika halafu (Amezaliwa Julai 27, 1982 Burundi au...) Babu, huo sio muundo wa makala za Wikipedia vile zinavyotakiwa ziwe! Unatakiwa uandike hivi:

Ukifanya hivyo utakuwa mmoja kati ya wanaofuata taratibu za uandikaji wa makala za Wikipedia! Kazi njema na kila la kheri. Nikiwa natokea Dar es Salaam, Tanzania, niite Muddyb Blast au-->>Mwanaharakati (Longa) 16:51, 15 Januari 2009 (UTC)[jibu]

Safi ndugu yangu! Habari za siku unajua kuna mambo mengi kwa kweli nikwa sababu ya muda lakini mitihani inakaribia kuisha nitakuuliza sana ila nitapendelea zaidi na wewe unisaidie maana nitatoa mchango zaidi katika mambo ya spoti maana ndio vitu hua ninafatilia sana. Kweli wakati hua naingia kwenye baadhi ya makali nilizofanya nakuona masahihisho baadhi kutoka kwako hua sipingi naninakubali makosa hayo ila ndio hivyo nitajitahidi nijikosei naninategemea nikimaliza exams nitatulia sana. Bwana baadhi ya makosa uwe unanisamehe ndugu yangu. Nakutakia kazi njema na maisha mema.

Miroslav Klose

[hariri chanzo]

Msafiri, salaaam! Nimeona umeanzisha makala ya jina tajwa hapo juu - halafu ukaiondosha maelezo yote kwenye eneo la makala. Baada ya muda nikafanya uchunguzi nikagundua ya kwamba umesahau kufunga mabano ya chini ya template infobox football player. Yaani hukufanya hivi mwishoni mwa template:

}}

Basi kila template inaanza na:

{{

Kisha inamalizia na:

}}

Na ndiyo maana wewe hukufaulu kulileta jedwali lile kwenye ramani yake! Basi nimesahihisha mawili matatu huku nikiwa nimeongezea maelezo kwenye makala ile! Ukijisikia kuongeza kitu kwenye makala hiyo, basi endelea wala usihofu Nd. yangu. Ni mimi wako mdogo, Muddyb Blast au niite--Mwanaharakati (Longa) 12:18, 10 Februari 2009 (UTC)[jibu]

Ndugu yangu kwa kweli nashukuru nanimeshaindikwa kwa urefu makala hiyo, ila nitaiweka karibuni hata namna yakuweka picha ndio nilikua nataka kuyafanya yote sababu kuna mtu alinipigia simu kuna jambo lilitoke ndio nikaenda kulifanya.

Kwa kweli nakushukuru sana ila nategemea nikimaliza nakuibandika itakufurahisha - nitaomba unisahihishe. Pia hata hii makala namna umeiandika hata kama ingali mbichi lakini umeiandika vizuri ndugu yangu. Nakutakia siku njema.

Pole na simu ulioipata! Haya, nimejaribu kufanya masahihisho mwanzoni kabisa mwa makala. Na kuhusu kusahihisho: Hilo litahitaji muda kwa kufuatia mimi mambo ya mpira sijui kabisaaa. Na wala sipendi huo mpira wenyewe, hivyo si rahisi kwangu kujua mengi au kusahihisha maneno ya mipira! Lakini nitajitahidi niiweke japo katika vijisehemu vomojavimoja ambavyo vitakuwa na utata. Karibu sana na kila la kheri huko uliko! Ahsante kwa kukuza Wikipedia yetu.--Mwanaharakati (Longa) 16:47, 10 Februari 2009 (UTC)[jibu]

Nimeshapoa ila nikitulia siku za usoni nitatoa mchango zaidi kuhusu mambo ya mpira wa miguu kutokana na ufatiliaji wangu kuhusu mambo hayo. Hamna tatizo katika mabadiliko yako ya juu ila nafikiri niliyapanga chini kidogo katika wasifu wake. Ninashukuru sana tena zaidi kwakunisahihisha maana nimeilimika baadhi ya mambo nikitulia zaidi nitatoa michango mingi lakini nitakutafuta na wewe pia unisaidie maana kuza yangu Wikipedia ya Kiswahili ni faida kwa watu wanauzungumza kiswahili.Kila la kheri.

Msafiri, salaaam! Nina jambo nataka kukumbia. Umeona katika ukurasa mmoja wa mtumiaji wa kuna kuwa na taratibu za kuweka lugha unazozijua! Kwa mfano wewe unaongea lugha ngapi na kwa kiwango gani? Tazama mifano:


Wikipedia:Babel
fr-3 Cet utilisateur peut contribuer avec un niveau avancé de français.
sw-3 Mtumiaji huyu anaweza kushiriki kwa Kiswahili cha kiwango cha juu.
en-2 This user is able to contribute with an intermediate level of English.
ar-1 هذا المستخدم يعرف مبادئ العربية.


Nimeweka Kifaransa mwanzo kwa sababu ninavyojua mie Waburundi wanaongea Kifaransa safi kabisa. Unachotakiwa kufanya ni kunakili maelezo haya:

{{Babel|sw-3|en-2|ar-1}}

Hapo unapoona nimeandika kifupi, mfano, sw-1,2,3, au 4 - ni kiwango cha lugha jinsi unavyoifahamu. Ukibadilisha namba 1,2,3 au 4, basi jua maandishi pia yatabadilika kutoka Msingi, Wastani, Juu, na Juu Kabisa! Mfumo huu unatumika katika kila lugha (kuna baadhi hazijawekwa bado). Lakini zile lugha kubwa-kubwa zipotayari! Ukitaka kujua zaidi namna ya kutumia kigezo cha lugha, basi angalia hapa! Ukiona umeshindwa kutumia hizi zana, basi nipe ruhusa ya kukuwekea katika ukurasa wako wa mtumiaji!!--Mwanaharakati (Longa) 06:26, 23 Mei 2009 (UTC)[jibu]


Bwana Muddyb Blast, Salaam! Hujambo lakini ? nategemea unaendelea salama na ndio furaha yangu, kwa kweli sasa hivi ndio ningali natoka kufanya mtihani University ndio nikasema acha nichungulie email nikaona ujumbe wako kwa kweli nimeshukuru sana nanimefurahi zaidi ila niko naelekea kumaliza exams siku za usoni nitajaribu nikutafute unionyeshe baadhi ya mambo katika ujenzi kwa ujumla kuhusu Wikipedia,Ama kuhusikana nakuniwekea hamna tatizo unaweza kuniwekea lakini anza Lugha ya Kiswahili Pili Kiarabu tatu Kiingereza usiweki Kifaransa maana hua kinanisumbua.

Na siku za usoni nitajitahidi nitizame namna ya kuweka picha katika zile makala nilizoandika bwana. Nakutakia kazi njema i was miss you maana ni siku nyingi.

Kuna kitu nimegundua. Siwezi kujua kiwango cha lugha unachoongea kwa upande wa Kiingereza na Kiarabu. Kwa upande wa Kiswahili, ninaweza kujua unaongea kiwango gani. Lakini kwa Kiingereza na Kiarabu, sipati picha... Je, unajua Kiarabu na Kiingereza kama jinsi unavyoongea Kiswahili?--Mwanaharakati (Longa) 11:23, 23 Mei 2009 (UTC)[jibu]

Ndugu yangu asante sana kwa hayo umenifanyia ila kwa kweli mitihani ndio inanisumbua zaidi nakuninyima muda, Ama kuhusikana na Kiarabu nakizungumza vizuri hata kiingereza pia nakipata sehemu kubwa lakini zote mbili nategemea siwezi linganisha na Kiswahili kwani Kiswahili nachukulia kua ndio lugha yangu ya kwanza, na Kiarabu nakizungumza vizuri kutokana na kukaa kwangu muda mrefu hapa Misri na Kiingereza pia nakipata kutokana na namna nakisomea hapa Chuo kikuu. Ninashukuru sana nitaomba jambo fulani kwako unisadie namna yakuweka picha kwenye Hi5 maana katika wachezaji nimeweka kuna baadhi yao wamesema watanitumia picha maana nafanya nao mawasilano kwenye Hi5 au email pia. Nakutakia kazi njema ndugu yangu.

Nimemteua Mwanaharakati achaguliwe kuwa msimamizi mkuu pamoja nasi (b'crat). Naomba upige kura kwenye ukurasa wa wakabidhi. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 07:20, 28 Mei 2009 (UTC)[jibu]

mradi wa Google kwa ajili ya wikipedia yetu

[hariri chanzo]

Bwana Msafiri, salaam!
Nimepata mawasiliano kutoka Christine Moon huko Palo Alto, California. Yeye anafanya kazi kwa shirika la Google, nao wameanza kupanga mradi au huduma kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania na Kenya ili waelimishwe kuandika makala kwa wikipedia ya Kiswahili. Kumbe!
Christine sasa ametualika kumwandikia maoni yetu, angalia tovuti hiyo:
http://docs.google.com/Doc?docid=0AbIPJ9Nv6udZZGd6MndwcGdfMzFkODNzOG0zYw&hl=en
Bahati mbaya yeye haelewi Kiswahili, kwa hiyo itakuwa lazima kumwandikia kwa Kiingereza. Ukihitaji msaada wangu upande wa kumwandikia, karibu unijulishe. Asante kwa michango yako!
Ni wako katika ujenzi wa lugha yetu, --Baba Tabita (majadiliano) 08:13, 10 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

majadiliano kuhusu utafsiri wa istilahi

[hariri chanzo]

Bwana Msafiri, salaam! Nimeanzisha majadiliano mapya kuhusu utafsiri wa istilahi ya wikipedia yetu hapa. Naomba uyaangalie na kuchangia maoni yako. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 10:06, 23 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]