Nenda kwa yaliyomo

Mohamed Zidan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muhamed Zidan
Maelezo binafsi
Jina kamili Muhamed Abdulla Zidan
Tarehe ya kuzaliwa 11 Desemba 1981
Mahala pa kuzaliwa    Port Said, Misri
Nafasi anayochezea Mshambuliaji
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Borussia Dortmund
Namba 10
Klabu za vijana
El-Masry
Timu ya taifa
2005 Misri

* Magoli alioshinda

Mohamed Abdulla Zidan (kwa Kiarabu: محمد عبدالله زيدان‎) (amezaliwa 11 Desemba,1981 katika mkoa wa Port Said, Misri) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka katika nchi ya Misri, ambae ni mshambuliaji katika klabu ya Ujerumani ya Borussia Dormund na pia katika timu ya taifa ya Misri.

Mohamed Zidan ni miongoni mwa wachezaji nyota wa Kimisri wanaocheza Ulaya, alianza kucheza mpira wa miguu akiwa katika umri wa myaka mi 8 katika Klabu ya Al-Misri Port Said huko Misri.

Maswala ya mpira[hariri | hariri chanzo]

Kuanza kwake kucheza mpira[hariri | hariri chanzo]

Mohamed Zidan alianza kucheza mpira katika klabu ya mkoa inayoitwa Al-Misri Port Said mwaka 1998-1999, lakini uchezaji wake haukuwakenaisha wakuu wa klabu hiyo ya Port Said, wakamuacha akiwa na miaka 16, akafika anajiunga na Klabu ya Jamarek (Katika Klabu za Ligi ya pili) na akaweza kuthibitisha nafsi yake kidogo kidogo nakuonekana kuwa mchezaji mzuri na akasaidia klabu yake kushika nafasi ya pili katika Ligi hiyo kwa mara ya kwanzi katika historia ya klabu hiyo nakuchukua ubingwa wa mfungaji magoli mengi katika ligi hiyo, japo kupendelea kwao.

Wakuu wa klabu hiyo ili Zidan kuendelea kuchezea klabu hiyo na ili waweze kuweka saini nae ili kuwa mchezaji wakulipwa ispokua matatizo ya kifamilia yaliharibu ili kijana aendelee kuchezea klabu hiyo, akahama yeye na familia yake katika nchi ya Denmark(Ulaya).

Katika maajabu yaliyotokea kwa Muhamed Zidan ni kujiunga katika Ligi ya Denmark, ni kuwa miongoni mwa makocha wa klabu ya AB Kopenhagen walimwona akicheza mechi zinazo kusanya watu wa tano huku na kule katika kauwanja kadogo wakampenda nakumchukua.

Akajiunga na klabu hiyo manmo mwaka 1999 hadi mwaka 2003 alishiriki Zidan na timu yake ya Kidenmark katika mechi 48 na akafunga magoli yapatayo 12. Hiyo ilimsaidia kabisa kuweza kujulikana Zidan katika ulimwengu wa mpira wa Ulaya.

Katika mwaka 2003 alihamia katika klabu nyingine huko huko Denmark inaitwa FC Midtjylland 2004, kwa hapo ndiyo akapata umashuhuri zaidi baada yakupata zawadi ya mchezaji bora katika Ligi ya Denmark katika mwaka wake wa kwanza alioshiriki na timu yake hiyo.

Alishiriki Zidan na FC Midtjylland katika mechi 47 alifunga magoli 30, kabla yakujiunga kwa kununuliwa kwa pesa nyingi katika klabu mashuhuri barani ulaya na ulimwengu ya huko Ujerumani ya SV Werder Bremen kwa njia ya kuazimwa kwa mwaka moja, na baadaye klabu hiyo ya Ujerumani ilimnunua moja kwa moja.

Alishiriki na klabu hiyo katika mechi 10 na alifunga magoli 2,baadaye klabu hiyo ikamwuza kwa njia yakuazima katika klabu ya Ujerumani nyingine inayoitwa 1. FSV Mainz 05 kunzia mwaka 2005 hadi 2006. Katika klabu hiyo alifunga magoli 10 katika mechi 30 na alionekana kuwa mchezaji mzuri tena alipendwa na washabiki wa timu hiyo hadi walitamani abaki ila haikuwezekana kwani Werder Bremen ikamuomba arudie kutokana na uchezaji wake mzuri ulionekana katika klabu hiyo ya Mainz.

Kutokufahamiana na kocha wa Werder Bremen: Zidan alikua hana uhusiano mzuri na kocha wa Bremen bwana Thomas Schaaf kutokana na kutokumshirikisha mara nyingi katika mechi baada ya kocha huyo kufadhilisha washambuliaji maarufu duniani kama vile Miroslav Klose (Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ujerumani) na Hugo Almeida (Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ureno)na Ivan Klasnic (Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kroatia).

Wakati huo Zidan alishiriki katika mechi 8 tu na akafunga magoli mawili katika kipindi cha mwaka 2006-2007 na ndio ikatokea timu ya Bremen kutangaza kumuuzisha,klabu ya Mainz ikafika inamnunua moja kwa moja kwa kiwango cha pesa milioni mbili na nusu za kizungu (Euro), na likua ni pesa nyingi kabisa tangu klabu hiyo kununua mchezaji.

Zidan alicheza vizuri katika klabu hiyo na alifunga magoli 13 katika mechi 15 lakini hakuwezi kuiokoa timu yake kutoteremka katika Ligi ya pili. Katika 30 Mei 2007 alijiunga na klabu ya Borussia Dormund (Ujerumani) kwa kiwango cha milioni tano za kizungu(Euro), akaendelea kuonekana uchezaji wake mzuri katika viwanja vya Ulaya. Kwa upande wa Timu ya Taifa:

Misri 2006[hariri | hariri chanzo]

Zidan hakushiriki katika timu ya Taifa ya Misri katika kombe la aina yoyote kwa mustawa wa kibara, hakucheza katika kombe la Afrika (mwaka 2006 Misri) kwa matatizo ya uumiaji, kama namna ulivyokua uchezaji wake wakucheza kwakujionyesha katika mechi za kirafiki ambazo alikua akishiriki na timu yake ya Taifa, jambo ambalo kocha wa Misri Hassan Shehata alifadhilisha wachezaji wengine ambao wanaocheza mpira wakipamoja kuliko kucheza kibinafsi.

Ghana 2008[hariri | hariri chanzo]

Ispokua Zidan alifuta kumbu kumbu zote ambazo sio nzuri kwa upande wa timu yake ya Taifa, katika kushiriki kwake kwa mara ya kwanza na timu yake ya taifa katika kombe la Afrika huko Ghana 2008, alisaidia sana timu yake ya taifa katika kuifunga Kameruni katika mechi hiyo alifunga magoli mawili katika magoli ma 4 kwakutumia umahiri na uchezaji wa pamoja. Jezi anayovaa katika timu ya taifa ni 9 katika klabu yake ni 10 nanikipenzi cha washabiki Misri.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]