Mtumiaji:Msafiri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wikipedia:Babel
sw-3 Mtumiaji huyu aweza kushiriki kwa Kiswahili cha kiwango cha juu.
en-2 This user is able to contribute with an intermediate level of English.
ar-1 هذا المستخدم يعرف مبادئ العربية.

Nzeyimana Msafiri Ruganyira (nimezaliwa tar. 5 mwezi wa 11 1982) katika mji mkuu wa Bujumbura, Burundi. Kwa sasa ninapatikana mjini Kairo, Misri kimasomo. Nilifika hapa Misri mwaka 1999, kwa sasa nazungumza lugha zifwatazo vizuri Kiswahili,Kiarabu, Kiingereza na Kihausa kidogo hizo lugha zote ndiyo ninazojifunza Chuo kikuu hapa Misri.


Mimi ni miongoni mwa watu ambao wanaotoa mchango wa baadhi ya makala muhimu katika Wikipedia ya Kiswahili. Kujiunga kwangu katika mchango huo ni kutokana na kutoa mchango wa kukuza lugha ya Kiswahili au kuwafikishia baadhi ya maalumati yanayohusu makala aina mbali mbali kwa wale wanaozungumza Kiswahili ili kupata urahisi wakuelewa baadhi ya vitu kwa upana.

Kiswahili ni lugha pana kabisa kwani hapa ninaposoma ninasoma na Wamisri ambao na wao pia wanazungumza Kiswahili, basi wanajifunza Kiswahili kwa njia yakusoma mambo fulani yaliyoandikwa kwa Kiswahili ili kukuza lugha uwezo wao wa kilugha. Ninategemea siyo hapa tu karibia sehemu zote ulimwenguni wale ambao wanaojifunza Kiswahili watapata fursa yakuisoma Wikipedia ya Kiswahili kwa njia yakufahamu baadhi ya mambo yanayohusu Kiswahili na kufahamu makala aina mbali mbali ambazo zitazungumzia mambo ya Kiafrika au ya Kiulimwengu.

Wakati nimejiunga katika Wikipedia hii nilipata uzito fulani katika baadhi ya mambo kuhusu kutengeneza makala lakini nilipata mtu anaroho nzuri yakusaidia au kwa njia nyingine anaependa ili wengine wasaidie katika kukuza wikipedia ya kiswahili nae ni bwana Muddyb Blast kaniraisishia ili niwe napangilia vizuri nanilifaanikisha kabisa ameniraisishia njia kabisa. Niliweza kutoa michango mingi katika kuandika makala aina mbali mbali katika Wikipedia ya Kiswahili na michango yenyewe hii hapa:

Wachezaji Mpira wa Miguu[hariri | hariri chanzo]

Waimbaji kutoka Burundi[hariri | hariri chanzo]

Wanasiasa na wanaharakati, Wanachuoni wa Kiislam[hariri | hariri chanzo]

Ali Muhsin al-Barwani Mwanasiasa mashuhuri na mwanachuoni wa Kiisalam kutoka Zanzibar