Majadiliano ya mtumiaji:Mary calist mlay
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
Kupitia Makala
[hariri chanzo]Salamu, hongera sana kwa juhudi zako katika kuhariri makala katika Wikipeida ya Kiswahili, sasa jaribu kupitia katika ukurasa wa mabadiliko ya karibuni, ama pitia katika makala ambazo umezianzisha kwa ajili ya kuona mabadiliko na maboresho mengine, ili utumie mfano huo katika kuboresha makala zako zitakazofuata, Amani sana Idd ninga (majadiliano)
Kuboresha makala
[hariri chanzo]Habari Mary, nimefurahi kuona kwamba unaendelea kusahihisha makala zako. Naona ni pia mazoezi mazuri kwa kujisikia nyumbani zaidi. Tafadhali angalia Uwanja_wa_michezo_wa_Derna uone masahihisho niliyofanya. angalia yafuatayo:
- Jamii: Kama "jamii:Viwanja vya Michezo Libya" bado ni nyekundi, haikuunganishwa bado na "Jamii:Viwanja vya michezo Afrika". (sasa itakuwa ni buluu, maana nimeunganisha). Hii unafanya kwa kubofya ile jami nyekundu, na kuingiza [[Jamii:Viwanja vya michezo Afrika]] (katika mabano mraba).
- Viungo: usisahau kuweka jina la nchi na pia jina la mji katika mabano mraba kama link. Kwa mji uone kama kuna zaidi ya moja kwa jina hilo, hapa utapeleleza kidogo na kusahihisha link (unajua namna?). Pia soka inafaa kuwa link, au aina nyingine ya michezo unayotaja (hapa utapeleleza tena inaitwaje kwetu)
- HERUFI KUBWA: uliandika DERNA kwa herufi kubwa. Hatutumii herufi kubwa lwa neno lote, isipokuwa kama ni jina rasmi au kifupi rasmi (UNESCO, CCM...)
- Tafsiri: ulikuwa na sentensi ya ajabu "Mechi na ni ardhi ya Darnes & Afriqi". Sasa ni lazima usome yote baada ya kumaliza. Ukiona sentensi ambayo si tena Kiswahili, angalia upya! Ukiona sentensi ya Kiingereza ambayo huelewi, usitafsiri . Au umwulize mtu maana yake ni nini. Hasahasa usitafsiri neno-kwa-neno, hii inaleta fujo mara nyingi. Wakisema kwa Kiingereza "the home ground ! basi ujiulize maana yake ni nini; hakika si "ardhi ya nyumbani". Usishangae, ni kawaida katika kutafsiri kwamba tunateleza, maana tunabadilisha fikra zetu kwenye muundo wa lugha nyingine. Ushauri mzuri ni: waza kwamba unasimulia habari zako mbele ya watoto wadogo. Wataelewa, je? Kipala (majadiliano) 07:11, 10 Juni 2021 (UTC)
Asante kwa kunirekebisha nitafanyia kazi.
Viungo vya Nje
[hariri chanzo]Hongera sana Mary kwa jitihada zako za kupitia mara kwa mara na kuziboresha makala katika Wikipedia, unapotaka kutafsiri neno External links kwa Kiswahili, ni bora kutumia kiswahili cha Viungo vya Nje kwa kuwa ndilo linalotumika sana huku,Twende kazi kwa pamoja, Amani sana Idd ninga (majadiliano)
Sawa Asante.
Marejeo - minara ya taa
[hariri chanzo]Habari, asante kwa kujitahidi, naona umefaulu kuingiza picha kwenye minara ya taa. Hongera. Lakini nimeona pia hujaweka marejeo ingawa marejeo yapo kwenye enwiki uliyotafsiri. Ila tu mara nyingi hawaweki tanbihi katika matini ya nakala mbali katika infobox ambayo hatupendi kugusa. Au tunakuta reference tata ambayo inaleta tanbihi nyekundu (yaani haifanyi kazi), mfano Mnara wa taa wa Nosy Alañaña (yaani marejeo yanayoonyesha kitu kama <refname= JINAFULANI> texttext<ref> au {{cite rowlett|mdg}} ambazo hazileti matokeo kwetu swwiki ukiizinakili).
Kama makala ya enwiki inaonyesha tanbihi (footnotes) chini ya makala, fanya hivi:
Fungua makala ya swwiki na pia ya enwiki. Kwenye makala ya enwiki fanya rightclick kwenye tanbihi (footnotes), ili upate tab 2 za tovuti zinazorejelewa. Hapo kopi URL na kuiweka kati ya mabano makali <ref>[xxxxxx yyyy]</ref>. xxxx ni URL unaokopi, yyyy ni matini ya tanbihi kutoka enwiki. Tunaweza njia hiyo badala ya ref tata zinazotokea mara nyingi kwenye enwiki.
Kwa njia hii huhitaji kufungua en-infobox, pia unaepukana na marejeo tata (pia utatambua kama marejeo ya enwiki ni "dead link")
Pia: External links: hizo tunakopi moja kwa moja kutoka skrini ya edit soure, isipokuwa tunabadilisha "Exteral links" kuwa "Vyanzo vya nje".
Mfano: nikiangalia en:Dona Amélia Lighthouse ambayo ulitafsiri, kuna "References" (=tanbihi au marejeo) na pia "External links" (Viungo vya nje) ambazo hujatumia katika swwiki. Si lazima kutafsiri yote tukichukua habari kutoka enwiki, lakini marejeo na vyanzo ni muhimu (kama zinalingana na matini unayotafsiri). Naomba upitilie tena kuziongeza. Kipala (majadiliano) 06:47, 17 Juni 2021 (UTC)
- sawa asante--Mary calist mlay (majadiliano) 07:11, 17 Juni 2021 (UTC)
Can you help me correct an article? Thank you!
[hariri chanzo]Hello, @Mary calist mlay:! I wrote an article on Andrea Benetti, a well-known Italian artist https://en.wikipedia.org/wiki/Andrea_Benetti_(artist). I used the automatic translator to make a draft https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:BarbaraLuciano13 . Could you help me correct the text and add the infobox with the photo at the beginning and the categories at the bottom? Unfortunately I don't know the language and I am not able to do it ... Thanks for what you can do, see you soon, --BarbaraLuciano13 (majadiliano) 09:11, 19 Juni 2021 (UTC)
Hongera, lakini uwe mwangilifu!
[hariri chanzo]NApenda kukupa hongera, naomba makala zako kwa jumla zinakaa vizuri siku hizi. Ila bado naomba jitahidi kuwa mwangilifu. Mfano katika Mnara wa taa wa Ponta do Norte umeingiza mnara wa Masonry - ambayo haina maana kabisa. Tafakari wanachotaka kusema; usipoelewa acha sentensi hiyo. Menginevyo utumie maneno yako mwenyewe. Nimweka "jengo la mawe".
pia: kamwe Viungo Vya >> iwe Viungo vya nje.
Naona bado unapambana na viungo tata (complex footnotes), umeacha tanbihi hii: {{|cpv|accessdate=15 August 2018}}. Hii ni kosa, ni rahisi kuepukana nayo. Ukiona kitu kama <ref name=rowlett>{{cite rowlett|cpv|accessdate=15 August 2018}}</ref>, usiikopi kamwe!!! Upande wa kiingereza kuna templates zinazoshughulika hayo ambayo hatuna kwa Kiswahili!
Fanya hivi: Kwenye makala ya Kiingereza, upande wa References, fanya rightclick kwa sehemu ya buluu, hivyo unafungua viungo vya chanzo chenyewe; hapa ni URL https://msi.nga.mil/api/publications/download?key=16694312/SFH00000/UpdatedPub113bk.pdf&type=view na https://www.ibiblio.org/lighthouse/cpv.htm .
Sasa unatumia URL hiyo; ukiwa kwenye "Hariri chanzo" utabofya alama halafu kuunda tanbihi (unajua jinsi gani?) Ukitumia "Chanzo" (visual edit) bofya Cite halafu Manual na kuchagua Basic. Pale unaweka URL juu na baada ya kuacha nafasi matini unayotaka kuonyesha katika tanbihi.
Naomba uthibitishe kwamba umeelewa. Halafu upitilie tena makala zote na kusahihisha hayo. Kipala (majadiliano) 16:36, 4 Julai 2021 (UTC)
Mary calist mlay (majadiliano)sawa asanteMary calist mlay (majadiliano)
Picha uliyochagua haina uhusiano na maziwa yale ya Kenya. Ni picha kutoka Marekani. Tafadhali tuwe waangalifu, maana majina mara nyingi yanaweza kurudiarudia mahali tofauti. Kipala (majadiliano) 07:33, 8 Julai 2021 (UTC)
```sawa asante```
Chanzo cha picha??
[hariri chanzo]Mary unapiga mbio sana lakini nimeshaona sasa mifano mingine kwamba umeteua picha ambayo haionyeshi mahali ulipohariri. Je unatafuta namna gani? Unatafuta commons kwa kutumia jina la makala ??? Kama ni vile tafadhali usiendelee. Hatari ni kuchanganya majina. Njia rahisi ni kufungua makala ye enwiki, au sasa ukihariri miji mingi ya Italia, itwiki. Uchague kutoka picha za huko. Unafungua tu makala ya enwiki, rightclick kwenye picha, inakupeleka kwenye makala. Kama hakuna picha (mfano Maziwa Carr) usijaribu kutafuta maana utapoteza muda na hatari ni kubwa unachanganya (kama kwenye mfano wa Maziwa Carr). Kipala (majadiliano) 18:23, 8 Julai 2021 (UTC)
```ninatoa picha commons na kwenye page ya kingereza, ila eben amesisitiza sasa nitoe kwenye makala za lugha nyingine```
- Tatizo la commons ni, a) wakati mwingine picha ni nyingi kwa hiyo inawezekana tunachagua picha isiyo nzuri sana, ilhali enwiki (au ukihariri miji ya Italia: Itwiki) kuna picha nzuri zaidi, halafu b) majina yanafanana hivyo tunachagua picha isiyo penyewe. naongeza hapa mifano kadhaa ambako nimeona picha ya mahali tofauti (2x) na menginevyo picha ambazo hazionyeshi kweli kitu cha maana (kwa mabano wapi kuna nzuri zaidi). Jambo dogo: naona umeandika mara kwa mara "italia" badala ya "Italia" chini ya picha.
- Putignano ????? ona itwiki
- Cascina wrong (inaonyesha Borgata Vittoria) ona itwiki
- Triggiano no pic, map ona itwiki
- Gravina di Catania wrong (inaonyesha mji wa Catania) ona itwiki, enwiki
- Caltagirone no pic, map ona itwiki
- Selargius ????? ona itwiki
- Mondragone ????? ona itwiki
- Kipala (majadiliano) 19:32, 8 Julai 2021 (UTC)
- Ninaongeza:
- Parisi wrong , inamwonyesha jenerali Parisi, si mtakatifu
- Iglesias wrong inaonyesha kanisa la Cala Cala ona itwiki
- Brugherio ????? ona itwiki
- Crema ????? ona enwiki
- Kimalay cha Visiwa vya Cocos wrong inaonysha eneo la bamba la gandunia, si eneo la lugha
- Falls Creek wrong inaonyesha Salmon Falls Creek , Australia ona enwiki
- Werner Schuster (mwanasiasa) wrong inamwonyesha mwigizaji Helmut Schuster, si mwanasiasa
- Clarksville, Tennessee ???? enwiki
- Ziwa Trasimeno wrong inaonyesha Como, Como Lake.jpg ona enwiki Kipala (majadiliano) 20:18, 8 Julai 2021 (UTC)
Kinihira
[hariri chanzo]Salamu, katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Kinihira umebandika picha ambayo inaonyesha miliki ya utawala wa Rwanda, lakini mkoa wa Kinihira hauonekani katika picha hiyo, hivyo pitia tena makala hiyo na kutazama kama picha hiyo inaendana kweli na makala iliyopo,Amani sana Idd ninga (majadiliano)
```habari Iddi asante ila nimetoa picha enwik ,ngoja niangalie tena``` ```alafu angalia vizuri kwenye hiyo ramani BYUMBA utaikuta KINIHIRA```
Ulaya ya Mashariki
[hariri chanzo]Katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya_ya_Mashariki inazungumzia ulaya ya mashariki lakini umeongeza picha ambayo inazungumzia Ukuaji wa Ukristo, badi picha hiyo hainyeshi mahusiano na makal iliyopo, ipitie, na kama kuna mapungufu yaondoe katika makala hiyo , Amani Sana Idd ninga (majadiliano)
Kukaribisha Wageni
[hariri chanzo]Habari ndugu nafurahi sana kwa kazi yako ya kutoa ukaribisho lakini unasahau ~~~ alam hizi zinapaswa kuwa nne tu ambazo zinatambulisha jina lako ukiweka alama nane haipendezi jina lako kutokea mara mbili Amani kwako Hussein m mmbaga (majadiliano) 15:37, 11 Julai 2023 (UTC)