Nenda kwa yaliyomo

Magdalene Odundo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Magdalene Anyango Namakhiya Odundo (alizaliwa Nairobi, 1950) ni Mwingereza mwenye asili ya Kenya anayeishi Franham[1]; alikuwa mkuu wa chuo katika chuo kikuu cha Sanaa cha University for the Creative Arts tangu mwaka 2018.[2]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Magdalene Odundo alipata elimu yake katika nchi ya India na Kenya. Mwaka 1971 alihamia Uingereza kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusu sanaa za utengenezaji wa picha baada ya kumaliza mafunzo alihamia Farnham, Surrey.[1] Odundo ni muhitimu wa wa sanaa katika chuo cha sanaa cha Cambridge School of Art,[3]ambapo alianza rasmi kuwa mtaalamu katika sanaa za utengenezaji wa bidhaa za Kauri.[4]

Kati ya miaka 1974 na 1975, baada ya kukaa kwa muda katika nchi ya Uingereza, aliamua kutembelea nchini Nigeria ambako alianza kujifunza na kufahamu zaidi kuhusiana na sanaa ya Ufinyanzi wakati alipotembelea katika kituo cha Pottery Training Centre katika jiji la Abuja, na kisha alirudi Kenya kwa ajili ya kujifunza mbinu za asili za uifnyanzi.[5]Magdalene alipata shahada ya sanaa katika chuo cha Royal College of Art mjini London. alifunisha katika chuo cha Commonwealth Institute kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1979 na chuo cha Royal College of Art kuanzia mwaka 1979 hadi 1982, kabla ya kurejea na kufundisha katika chuo cha Surrey Institute of Art & Design (kwa sasa ni chuo kikuu cha Ubunifu wa Sanaa) mwaka 2001 alikuwa profesa katika masuala ya sanaa.

Maisha ya kazi

[hariri | hariri chanzo]
Vase, 1990, Brooklyn Museum

Kazi bora ya Odundo inayojulikana sana ni ile aliyoitengeneza kwa mikono yake na kwa ufundi wa ufinyanzi na kuchomwa kitaalamu.

Mnamo Agosti 29, 2021, sufuria ya udongo ya Magdalene Odundo mnamo 1986 iliuzwa kwa € 440,000 kwenye mnada.[6]

  1. 1.0 1.1 Khanchandani, Priya. "Magdalene Odundo: 'Of all mediums, clay is the most versatile, pliable and human'", 17 August 2019. 
  2. "World-renowned ceramicist becomes Chancellor of the University for the Creative Arts". University for the Creative Arts. 25 Juni 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-09. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2020. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Joris, Yvonne G. J. M. (1994). Magdalene Odundo. Cip-Gegevens Koninklijke Bibliotheek, Den Haag. uk. 68.
  4. Morris, Tom (14 Februari 2019). "A new exhibition celebrates the global sweep of Kenya-born British artist Magdalene Odundo". Wallpaper. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Spring, Chris (2008). Angaza Afrika: African Art Now. London: Laurence King. ku. 234. ISBN 978-1-85669-548-0.
  6. "440 000 euros pour un pot de terre de Magdalene Odundo". Jeune Afrique. 02 September 2021. Iliwekwa mnamo 03 September 2021. {{cite web}}: Check date values in: |access-date= na |date= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Magdalene Odundo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.