Abuja
Jiji la Abuja | |
Nchi | Nigeria |
---|
Abuja ni mji mkuu wa Nigeria. Idadi ya wakazi wake imekadiriwa kuwa watu 178,462 [1]. Mwaka wa 1976, serikali ya Nigeria iliamua kuanzisha mji mkuu mpya badala ya Lagos. Wakachagua katikati ya nchi, na mipango ya ujenzi ikaundwa chini ya makampuni matatu ya Marekani: PRC Corporation; Wallace, McHarg, Roberts na Todd; na Archisystems. Mipango hiyo ikabadilishwa baadaye na Kenzo Tange, msanifu majengo maarufu wa Japani. Abuja ikatangazwa rasmi kuwa mji mkuu wa Nigeria tarehe 12 Desemba 1991. Iko mahali pa 9, 10, Kaskazini na 7, 10, Mashariki. [2] Ilihifadhiwa 25 Machi 2011 kwenye Wayback Machine.
Balozi za nchi nyingi zikahamishwa Abuja kutoka Lagos.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Sifa muhimu ya Abuja ni Mlima wa Aso ambao ni mwamba ulio na urefu wa mita 400. Upande wa kusini wa mlima huo, kuna Ikulu ya Rais, Bunge la Nigeria, Mahakama Kuu na sehemu nyingi za mji.
Majengo maarufu mengine ni Msikiti wa Taifa (Nigerian National Mosque) na Kanisa Kuu la Madhehebu (National Ecumenical Centre Cathedral). Kuna kiwanja cha ndege cha kimataifa (Nnamdi Azikiwe International Airport), karibu na Mlima wa Zuma. Sehemu nyingine za mji hazijajengwa ilivyopangwa, na majengo mengi yanaendelea kujengwa.
Mji wa Abuja unagombea kuwa mahali pa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa mwaka wa 2014 (2014 Commonwealth Games).
Marejeo ya nje
[hariri | hariri chanzo]- Official site of Nigeria's Federal Capital Territory (FCT) and City of Abuja Ilihifadhiwa 9 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.
- Makala ya WorldPress inayohusu mabadiliko kwenye Abuja Ilihifadhiwa 27 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Abuja Bid Announcement Ilihifadhiwa 11 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Picha za Abuja Ilihifadhiwa 26 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine.