Uainishaji wa kisayansi : Tofauti kati ya masahihisho
No edit summary |
No edit summary |
||
Mstari 1: | Mstari 1: | ||
[[Picha:Uainishaji.png|right|thumb|150px|Ngazi za uainishaji katika biolojia; ngazi ndogo za kati hazionyeshwi]] |
[[Picha:Uainishaji.png|right|thumb|150px|Ngazi za uainishaji katika biolojia; ngazi ndogo za kati hazionyeshwi.]] |
||
⚫ | |||
⚫ | |||
⚫ | |||
⚫ | |||
⚫ | |||
⚫ | |||
⚫ | |||
⚫ | |||
== Majina ya Kisayansi == |
== Majina ya Kisayansi == |
||
Kila spishi ya viumbehai inapewa jina la kisayansi lenye maneno mawili kufuatana na muundo wa uainishaji. Jina la Kisayansi linaanza kwa kutaja [[jenasi]] inayoandikwa kwa herufi kubwa halafu neno la pili kama sehemu |
Kila spishi ya viumbehai inapewa [[jina la kisayansi]] lenye [[neno|maneno]] mawili kufuatana na muundo wa [[uainishaji]]. Jina la Kisayansi linaanza kwa kutaja [[jenasi]] inayoandikwa kwa [[herufi]] kubwa, halafu neno la pili kama sehemu maalumu ya jina la spishi ile. Maneno hayo huandikwa kwa [[herufi za italiki]]. Kwa mabano hufuata jina la mtaalamu wa spishi pamoja na [[mwaka]] alioandika maelezo yake. |
||
Kwa mfano [[paka]] anaitwa ''Felis silvestris'' (Linnaeus, 1758) na spishi hii inajumlisha paka wa porini na paka wa nyumbani. |
Kwa mfano [[paka]] anaitwa ''Felis silvestris'' (Linnaeus, [[1758]]) na spishi hii inajumlisha paka wa porini na paka wa nyumbani. |
||
* [[Felis]] ni jina la jenasi. Jenasi huandikwa kwa herufi kubwa. |
* [[Felis]] ni jina la jenasi. Jenasi huandikwa kwa herufi kubwa. |
||
* "silvestris" ni sehemu ya pili |
* "silvestris" ni sehemu ya pili ya neno; linasema "wa msituni" kwa sababu inaaminiwa ya kwamba asili ya paka hizi zote ni aina ya paka wa porini wa [[Asia]], [[Ulaya]] na [[Afrika Kaskazini]]. |
||
Paka wa nyumbani anayefugwa na watu |
Paka wa nyumbani anayefugwa na watu anatazamwa kama [[nususpishi]], na nususpishi hii inaweza kutofautishwa kwa kuongeza neno la tatu "catus" kuwa "''Felis silvestris catus''". Hili ni jina la nususpishi ya paka wanaofugwa na [[watu]]. Nususpishi hii ina aina nyingi ndani yake, kutokana na [[ufugaji]] na [[uteuzi]] lakini zote zimo ndani ya nususpishi ileile. |
||
Hili ni jina la nususpishi ya paka wanaofugwa na watu. Nususpishi hii ina aina nyingi ndani yake kutokana na ufugaji na uteuzi lakini zote zimo ndani ya nususpishi ileile. |
|||
Katika mabano lipo jina la mtaalamu aliyeeleza spishi hii mara ya kwanza kwa namna ya kisayansi pamoja na mwaka alipoandika. Katika mfano wa paka ni Carolus Linnaeus anayefupishwa mara nyingi kama "L.". Aliandika kitabu chake mwaka [[1728]]. |
Katika mabano lipo jina la mtaalamu aliyeeleza spishi hii mara ya kwanza kwa namna ya kisayansi pamoja na mwaka alipoandika. Katika mfano wa paka ni Carolus Linnaeus anayefupishwa mara nyingi kama "L.". Aliandika [[kitabu]] chake mwaka [[1728]]. |
||
== Umbo la majina katika uinishaji == |
== Umbo la majina katika uinishaji == |
||
Katika |
Katika uainishaji wataalamu wamepatana jinsi ya kutumia majina kwa ngazi mablimbali. Umbo la majina haya hufuata [[sarufi]] ya [[Kilatini]]. |
||
{| class=wikitable |
{| class=wikitable |
||
Mstari 86: | Mstari 84: | ||
[[Jamii:Uainishaji]] |
[[Jamii:Uainishaji]] |
||
[[Jamii:Biolojia]] |
Pitio la 14:27, 7 Februari 2016
Uainishaji wa kisayansi ni jinsi wataalamu wa biolojia wanavyopanga viumbehai kama mimea na wanyama kwa vikundi kwenye ngazi mbalimbali. Inaweza kuitwa pia taksonomia.
Tangu muda mrefu watu walitambua ya kwamba wanyama au mimea mbalimbali wanafanana kati yao kwa namna moja au nyingine. Wataalamu walijaribu kupanga aina hizo kwa vikundi vyenye tabia za pamoja. Carolus Linnaeus alianza kuzipanga kwa muundo ulioeleweka kulingana na tabia za maumbile yao.
Mfumo wa Linnaeus uliendelezwa baadaye kulingana na nadharia ya Charles Darwin inayoona ya kwamba spishi mbalimbali huwa na chanzo cha pamoja, kwa hiyo inawezekana kupanga uhai wote kama mti yenye matawi makubwa, tena madogo yanayotoka kwenye makubwa.
Ujuzi wa kisasa kutokana na utafiti wa DNA ndani ya seli za viumbehai unaendelea kuongeza ujuzi wetu kwa hiyo katika mengi uainishaji ni utaalamu unaozidi kubadilika.
Majina ya Kisayansi
Kila spishi ya viumbehai inapewa jina la kisayansi lenye maneno mawili kufuatana na muundo wa uainishaji. Jina la Kisayansi linaanza kwa kutaja jenasi inayoandikwa kwa herufi kubwa, halafu neno la pili kama sehemu maalumu ya jina la spishi ile. Maneno hayo huandikwa kwa herufi za italiki. Kwa mabano hufuata jina la mtaalamu wa spishi pamoja na mwaka alioandika maelezo yake.
Kwa mfano paka anaitwa Felis silvestris (Linnaeus, 1758) na spishi hii inajumlisha paka wa porini na paka wa nyumbani.
- Felis ni jina la jenasi. Jenasi huandikwa kwa herufi kubwa.
- "silvestris" ni sehemu ya pili ya neno; linasema "wa msituni" kwa sababu inaaminiwa ya kwamba asili ya paka hizi zote ni aina ya paka wa porini wa Asia, Ulaya na Afrika Kaskazini.
Paka wa nyumbani anayefugwa na watu anatazamwa kama nususpishi, na nususpishi hii inaweza kutofautishwa kwa kuongeza neno la tatu "catus" kuwa "Felis silvestris catus". Hili ni jina la nususpishi ya paka wanaofugwa na watu. Nususpishi hii ina aina nyingi ndani yake, kutokana na ufugaji na uteuzi lakini zote zimo ndani ya nususpishi ileile.
Katika mabano lipo jina la mtaalamu aliyeeleza spishi hii mara ya kwanza kwa namna ya kisayansi pamoja na mwaka alipoandika. Katika mfano wa paka ni Carolus Linnaeus anayefupishwa mara nyingi kama "L.". Aliandika kitabu chake mwaka 1728.
Umbo la majina katika uinishaji
Katika uainishaji wataalamu wamepatana jinsi ya kutumia majina kwa ngazi mablimbali. Umbo la majina haya hufuata sarufi ya Kilatini.
Ngazi | Mimea (planta) |
Mwani (algae) |
Nyoga (fungi) |
Wanyama (animalia) |
---|---|---|---|---|
Faila | -phyta | -mycota | ||
Nusufaila | -phytina | -mycotina | ||
Ngeli | -opsida | -phyceae | -mycetes | |
Nusungeli | -idae | -phycidae | -mycetidae | |
Oda ya juu | -anae | |||
Oda | -ales | |||
Nusuoda | -ineae | |||
Familia ya juu | -acea | -oidea | ||
Familia | -aceae | -idae | ||
Nusufamilia | -oideae | -inae | ||
Kabila | -eae | -ini | ||
Nusukabila | -inae | -ina |
Makala Biolojia bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |