Nyuki : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Masahihisho
dNo edit summary
Mstari 29: Mstari 29:


== Wadudu wa kijamii ==
== Wadudu wa kijamii ==
Spishi kadhaa za nyuki ni wadudu wa kijamii maana yake wanaishi katika kundi si peke yao kama aina nyingine za nyuki. Wanajenga [[sega]] ya [[nta]] ndani ya [[mzinga wa nyuki]] na humu wanatunza asali [[yao]].
Spishi kadhaa za nyuki ni wadudu wa kijamii maana yake wanaishi katika kundi si peke yao kama aina nyingine za nyuki. Wanajenga [[sega]] ya [[nta]] ndani ya [[mzinga wa nyuki]] na humu wanatunza asali yao.


Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi na mzinga wao ambao ni
Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi na mzinga wao ambao ni

Pitio la 18:57, 17 Julai 2013

Nyuki
Kike wa nyuki-mbao (Xylocopa caffra)
Kike wa nyuki-mbao (Xylocopa caffra)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba sana)
Familia: Apidae (Wadudu walio na mnasaba na nyuki)
Ngazi za chini

Nusufamilia 3:

Nyuki ni wadudu wa familia Apidae wenye mabawa manne angavu na mwiba kwenye nyuma ya mwili wao wanaokusanya mbelewele na mbochi ya maua kama chakula chao. Spishi inayojulikana hasa ni nyuki-asali (Apis mellifera) ambaye hufugwa kila mahali duniani. Kuna spishi zaidi ya 20,000 zinazojumlishwa na biolojia kati ya nyuki lakini ni wale wa jenasi Apis wanaotengeneza asali inayovunwa na wanadamu.

Mwili wa nyuki

Mwili wa nyuki

Mwili una pande tatu jinsi ilvyo kwa wadudu wote: kichwa mbele, kidari katikati na tumbo nyuma, halafu jozi tatu za miguu na jozi mbili za mabawa.

Mwili huwa na nywele na ina rangi kali za njano-nyeusi kama onyo dhidi ya maadui.

Nyuma ya tumbo wanabeba mwiba wanaotumia kudunga wakijisikia wameshambuliwa. Wakidunga mwiba wanaingiza pia kiasi kidogo cha sumu katika kidonda. Sumu hii inasababisha maumivu na watu wengine wanaathiriwa vikali lakini si kila mtu. Kuna nyuki wanaokufa baada ya kudunga kwa sababu mwiba unabaki kwenye kidonda lakini wengine wanaweza kutoa mwiba na kudunga tena.

Wadudu wa kijamii

Spishi kadhaa za nyuki ni wadudu wa kijamii maana yake wanaishi katika kundi si peke yao kama aina nyingine za nyuki. Wanajenga sega ya nta ndani ya mzinga wa nyuki na humu wanatunza asali yao.

Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi na mzinga wao ambao ni

  • malkia wa nyuki ni mama wa nyuki wote ndani ya kundi na kazi yake ni kutaga mayai pekee
  • nyuki wafanyakazi ni wakazi wengi wa mzinga na wote ni wa kike. Ni hao wanaofanya kazi yote kama kukusanya mbelewele na mbochi, kusafisha mzinga, kutengeneza nta, kujenga sega, kumlisha malkia na majana, kultetea mzinga
  • nyuki dume ni wachache na kazi yao ya pekee ni kukwea malkia lakini si yule wa mzinga wake kwa kawaida; baadaye wanafukuzwa kwenye mzinga na hawapewi chakula tena
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyuki kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.