Nenda kwa yaliyomo

Lupo wa Troyes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Lupo.

Lupo wa Troyes (pia: Loup, Leu; Toul, leo nchini Ufaransa, 383 hivi - Troyes, leo nchini Ufaransa, 479 hivi) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 426, baada ya kuishi miaka 6 katika ndoa halafu katika monasteri ya Lerins.

Alipambana na uzushi wa Upelaji hata kwa kwenda Britania pamoja na askofu mwenzake Jermano wa Auxerre.

Kwa sala zake alilinda salama mji wake dhidi ya uvamizi wa Attila akafariki baada ya miaka 52 ya upadri[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Julai[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Lupus of Troyes
  • Index of Saints website with thousands of saints, and sources. (an archived, earlier version of "Saint of the Day" at www.saintpatrickdc.org)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.