Nenda kwa yaliyomo

Upelaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mzushi Pelagius na Yohane Krisostomo katika Nuremberg Chronicle, 1493

Upelaji (kwa Kiingereza: Pelagianism) ni mtazamo wa teolojia ya Ukristo unaodhani dhambi ya asili haijaharibu umbile la binadamu, hivyo hiari yake inaweza bado kutekeleza maadili bila kuhitaji neema ya pekee kutoka kwa Mungu. Hatimaye mtu anaweza kujipatia wokovu kwa juhudi zake mwenyewe.

Mtazamo huo umepata jina kutokana na mmonaki wa Ireland[1] Pelagius (354420 au 440), ingawa pengine huyo alikataa baadhi ya mafundisho yaliyosemekana kuwa yake.

Ulipingwa hasa na Agostino wa Hippo na kulaaniwa na mtaguso wa Kartago wa mwaka 418, halafu na mtaguso wa Efeso (431).

Hata hivyo unajitokeza tena na tena katika historia ya Kanisa, hasa katika makundi yenye juhudi katika maisha ya Kiroho kama upelajiupande.

  1. H. Zimmer (1901). "Pelagius in Ireland". Berlin. uk. 20.{{cite book}}: CS1 maint: location missing publisher (link)
  • Bercot, David. A Dictionary of Early Christian Beliefs, Hendrickson Publishers
  • Rees, B. R., The Letters of Pelagius and his Followers, The Boydell Press

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]
Maandishi ya Pelagius

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Upelaji kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.