Nenda kwa yaliyomo

Kiwavijeshi bandia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Leucania loreyi)
Kiwavijeshi bandia
Mdumili wa kiwavijeshi bandia kutoka juu
Mdumili wa kiwavijeshi bandia kutoka juu
Mdumili wa kiwavijeshi bandia kutoka chini
Mdumili wa kiwavijeshi bandia kutoka chini
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Lepidoptera (Wadudu walio na mabawa yenye vigamba)
Nusuoda: Glossata {Lepidoptera wenye ulimi unaoweza kuviringwa)
Familia ya juu: Noctuoidea (Nondo kama nondo wa nyanya)
Familia: Noctuidae (Nondo walio na mnasaba na nondo wa nyanya)
Nusufamilia: Hadeninae (Nondo wanaofanana na viwavijeshi)
Jenasi: Leucania
Ochsenheimer, 1816
Spishi: L. loreyi
Duponchel, 1827

Viwavijeshi bandia ni viwavi wa nondo Leucania loreyi katika familia Noctuidae. Viwavi hao hawatembei chanjari kama viwavijeshi wa Afrika na wadumili hawahami mbali kubwa katika makundi makubwa. Hata hivyo viwavi hao wanaweza kulipuka na kufunika uoto kwa wengi kama jeshi.

Viwavi wadogo ni weusi au kahawia na hatua zifuatazo ni kahawiakijivu zenye milia miwili myeupe hadi hudurungi. Kiwavi wa hatua ya mwisho ana urefu wa takriban mm 35. Wadumili wana urefu wa mm 15-20. Mabawa ya mbele ni hudurungi yenye doa jeusi katikati. Mabawa ya nyuma ni meupe yenye vena hudurungi.

Wadumili hukiakia wakati wa usiku. Majike hutaga zaidi ya mayai 1000 juu ya bua na majani. Viwavi wanaotoka katika mayai hula matabaka ya juu ya tishu za majani ambayo inabakiza vidarisha katika majani. Viwavi walio wakubwa zaidi hula majani mazima lakini pengine hubakiza neva kubwa za majani. Wakikomaa huanguka chini na kuunda mabundo ardhini.

Viwavi hao hula spishi za nyasi hasa, k.m. mpunga, ngano, shayiri, mhindi, mtama, muwa na tete. Mara kwa mara wanaweza kuwa waharibifu kiasi.

Udhibiti

[hariri | hariri chanzo]

Wakulima wengi hutumia viuawadudu vya kikemikali, lakini inapendekezwa kutumia dawa za kibiolojia, kama vile Bt, ili kuhifadhi maadui ya asili. Hao wanajumuisha nyigu na nzi vidusia, sisimizi, wadudu-kibibi na kunguni-mgunda mbuai. Viwavi wanaweza kuambukizwa pia na virusi.