Nenda kwa yaliyomo

Nondo (mdudu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Glossata)

Kwa maana nyingine za jina hili tazama nondo (maana)

Nondo
Nondo-bundi (Cyligramma latona)
Nondo-bundi (Cyligramma latona)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Lepidoptera (Wadudu walio na mabawa yenye vigamba)
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Nusuoda 5:

Nondo ni wadudu wa oda ya Lepidoptera (lepidos = gamba, ptera = mabawa) ambao wanabeba vigamba juu ya mabawa yao. Nondo wanafanana na vipepeo lakini wanatofautiana kwa umbo la vipapasio. Vile vya vipepeo ni kama nyuzi zenye kinundu mwishoni kwao lakini vile vya nondo vina maumbo mbalimbali bila kinundu. Juu ya hiyo takriban nondo wote hukiakia wakati wa usiku na vipepeo hukiakia wakati wa mchana. Kuna zaidi ya spishi 160,000 za nondo.

Utangulizi

[hariri | hariri chanzo]

Kama ilivyo kwa vipepeo mzunguko wa maisha wa nondo huwa na hatua nne: yai, kiwavi (lava), bundo na mdumili (imago). Takriban spishi zote huruka wakati wa usiku lakini nyingine huruka jioni na spishi kadhaa wakati wa mchana. Mabawa yakiwa yamefungwa rangi za nondo ni kahawia na/au kijivu hasa na mara nyingi wana rangi za kamafleji. Lakini wakifungua mabawa yale ya nyuma yana rangi kali mara nyingi au mabaka yanayofanana na macho. Hii inashtua mbuai wao kama ndege na mijusi.

Takriban wadumili wote wa nondo hawali, lakina kadhaa hula mbochi. Viwavi vya spishi nyingi vinakula mimea ya mazao. Kwa kawaida wakulima hutumia dawa za kikemikali kuua viwavi hivi. Lakini siku hizi vimekuwa sugu dhidi ya dawa hizi. Kwa hivyo ni bora kutumia dawa za kibiolojia, kama Bt au virusi au kuvu viuawadudu.

Katika sehemu mbalimbali za Afrika viwavi vya spishi kubwa huliwa, k.m. nondo wa mopani katika Afrika Kusini, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Namibia, Zambia na Zimbabwe.

Spishi kadhaa za Afrika

[hariri | hariri chanzo]