Mhindi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mhindi (muhindi)
(Zea mays subsp. mays)
Mhindi
Mhindi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja tu)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama kongwe)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Mimea iliyo na mnasaba na nyasi)
Jenasi: Zea
Spishi: Z. mays
L.


Zea mays "fraise"
Zea mays "Oaxacan Green"

Mhindi (pia: muhindi) ni mmea wa familia ya manyasi katika ngeli ya monokotiledoni. Mbegu za mhindi ni mahindi ambayo ni chakula muhimu katika sehemu nyingi za dunia pamoja na Afrika ya Mashariki na Afrika ya Kusini.

Asili ya muhindi[hariri | hariri chanzo]

Mhindi ni kati ya nafaka ya kwanza kulimwa kama chakula cha binadamu. Asili yake ni Amerika ya Kati ulipogundiliwa na Maindio. Wahispania walipeleka nafaka hii Ulaya; taarifa za kwanza za mashamba ya muhindi katika Hispania zilipatikana mwaka 1525 yaani miaka michache tu baada ya safari ya Kolumbus.

Katika Afrika mmea huu ulifika kupitia Wareno. Jina la muhindi/mhindi ni kumbukumbu ya imani ya Wazungu ya kuwa Kolumbus alifika Uhindini ya Asia na Wahispania pamoja na Wareno waliendelea kuita nchi mpya "India" kwa miaka mingi. Hivyo nafaka kutoka "India" ile iliingia katika Kiswahili kwa jina lililolingana na imani ya Wareno kuhusu asili yake. Jina hili ni sawa na jina la Kifaransa "froment des Indes" (ngano ya Uhindi). Lakini katika nchi nyingi jina la Kihispania la "maiz" limeenea kutoka neno la Kiindio "mahiz" katika lugha ya taino kwenye kisiwa cha Haiti.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Muhindi ni nafaka inayolimwa kwa wingi zaidi duniani. Mavuno ya dunia ya mwaka 2005 yalileta matokeo yafuatayo: mahindi tani milioni 710.3; mchele tani milioni 628.5 na ngano tani milioni 620.0.

Sababu ya kupendelea muhindi ni kivuno kikubwa. Dunia muhindi inaleta kwa wastani mahindi tani 47.5 kwa hektari moja. Hii inashinda mpunga unaoleta mchele wastani tani 40/ha na ngano yenye tani 29/ha.

Kwa jumla kuna tofauti katika matumizi: - nchi za viwanda hulima muhindi hasa kama chakula cha wanyama; hapa mhindi wote huvunwa ukitumiwa kama sileji. - nchi zinazoendelea hutumia zaidi mahindi yaani nafaka yake kama chakula cha kibinadamu.


Greentree.jpg Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mhindi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.