Lego

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Matofali ya Lego
Mfano wa Trafalgar Square (London) huko Legoland

Lego ni jina la kampuni nchini Denmark inayoteneneza vichezeo mashuhuri ya "Lego". Kampuni ni mtengezaji mkubwa wa vichezeo duniani.

Matofali ya plastiki[hariri | hariri chanzo]

Lego ni hasa matofali madogo ya plastiki yanayoweza kuunganishwa kuunda mifano ya kila kitu.

Kiasili kampuni ilitengeneza michemraba ya ubao na tangu 1949 mtindo huu ulipanushwa kwa kutumia plastiki. Baada ya kufaulu chaguo la vipande za kuunganishwa liliongezeka kuwa pamoja na mwanaserere ndogo[1], na magurudumu na vipande vingine kwa kuunda gari. Kuna pia mikusanyo ya vipande vya nyongeza vinavyorihusu kuunda mifano ya miji, anga la nje, jahazi na meli, maboma, masauri, na mengi mengine.

Lego Technic[hariri | hariri chanzo]

Tangu 1977 Lego ilipanushwa kwa vipande vya Lego Technic iliyoongeza injini za umeme, kompresa na pampu za hewa zilizoruhusu kuunda mifano ya trekta au mashine mengine.

Roboti za Lego[hariri | hariri chanzo]

Mtindo huu umepanishwa katika karne mpya kwa vipande vya "Lego Mindstorm" vinavyoruhusu kutengeneza roboti. Kiini chake ni tofali lenye chipu ndani yake inayopokea amri kupitia kompyuta ya nyumbani na amri zinatekelezwa kwa kutumia injini ya umeme na vigunduzi mbalimbali vya nuru, sauti na mgusano.

Kampuni ilianzisha pia miradi ya kitalii ya Legoland ambako mifano ya majengo mashuhuri ya dunia yanaonyeshwa ambayo yameundwa kwa matofali ya Lego.

Mifano ya matumizi ya Lego[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. zenye kichwa, mwili wa juu na mwili wa chini pekee, hivyo zinaweza kutenganishwa na kuunganishwa upya

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]