Nenda kwa yaliyomo

Lameck Ditto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lameck Ditto
Jina la kuzaliwa Dotto Bernad Bwakeya
Pia anajulikana kama "Lameck Ditto"
Amezaliwa 8 Januari 1987 (1987-01-08) (umri 38)
Asili yake Kagera/Morogoro, Tanzania
Aina ya muziki Zouk
Soul
Kazi yake Mwimbaji
Mwanamuziki
Mtunzi wa nyimbo
Mtayarishaji
Ala Ngoma
Sauti
Miaka ya kazi 2000 - hadi leo
Ame/Wameshirikiana na Afande Sele<r>Mrisho Mpoto
Watupori
Tovuti http://www.lameckditto.com

Dotto Bernad Bwakeya (a.k.a Lameck Ditto) ni mwimbaji wa muziki wa Bongo Flava aliyetambulika na rapa mkongwe Afande Sele mwaka 2003 katika tamasha la kuibua vijana wadogo wenye vipaji lililoandaliwa na i kituo cha Redio Ukweli kilichokuwa na makao yake Morogoro, Tanzania.

Wakati huo akiitwa Dogo Ditto, alishirikishwa katika nyimbo zote za albamu ya pili ya Afande Sele, Darubini Kali, ikiwemo wimbo maarufu wa Darubini Kali. Mwaka 2004, Lameck Ditto alimshirikisha Afande Sele katika wimbo wake wa kwanza akiwa msanii anayejiendeleza peke yake, Dunia Inamambo, ambao ulifanya vizuri na kutamba katika chati za Afrika Mashariki. Mwaka 2005, Lameck Ditto, akiwa na Afande Sele na MC Koba, alianzisha kundi la Watupori baada ya kundi la Ghetto Boys kuvunjika.

Watupori, lililokuwa na makao yake Morogoro, lilifanikiwa kutoa nyimbo kama Usinichukie, Nafsi ya Mtu, na Sana Tu, ambazo zilivuma na kushika nafasi za juu kwenye chati. Hata hivyo, kundi hilo halikudumu kwa muda mrefu kutokana na migogoro, na inasemekana kwamba Lameck Ditto alihusishwa na mvutano wa kibiashara baada ya kutakiwa na Bongo Records ya P Funk, ambaye alitaka kumpatia mkataba wa kurekodi albamu yake ya peke yake nje ya Watupori [1].

Lameck Ditto na MC Koba waliondoka kwa Afande Sele na kuungana na kurekodi albamu yao ya kwanza katika studio za Bongo Records. Walifanikiwa kutoa wimbo wa Ulibisha Hodi, ambao ulifanya vyema kabla ya wote kujiunga na kundi la LaFamilia, lililokuwa likiongozwa na Chid Benz na lililojumuisha wasanii kama Kassim Mganga, Tunda Man, O Ten, Chiku Ketto, na MC Koba. Hapo ndipo Lameck Ditto alipoanza rasmi kutumia jina lake la Lameck Ditto. Katika La Familia, alishirikishwa katika nyimbo kama Ngoma Itambae (Dar es Salaam Stand Up) na Muda Umefika ft. Chiku Ketto.

Mwaka 2008, Ditto alijiunga na Taasisi ya Kukuza na Kulea Vijana wenye Vipaji ya Tanzania House of Talent (THT) ili kuongeza ujuzi wake katika fani hii. Aliweza kutoa nyimbo kama Wapo, Tushukuru Kwa Yote, na Niamini.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. "www.eastafricantube.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-06-24. Iliwekwa mnamo 2013-08-29.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lameck Ditto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.