Chid Benz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Chid Benz
Jina la kuzaliwa Rashidi Abdallah Makwiro
Pia anajulikana kama Chuma Cha Ilala
Amezaliwa 1985
Aina ya muziki Hip Hop,Gangsta Rap,Bongo Flava,RnB
Kazi yake Rapa
Ala Sauti
Ame/Wameshirikiana na LA Familia,Chiku k, Nikki Mbishi, One The Incredible

Rashidi Abdallah Mohamed Makwiro[1] (amezaliwa 1985) ni rapa wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania. Anafahamika sana kwa jina la kisanii kama Chid Benz. Yeye ndiye mwanzilishi na ndiye kiongozi wa kundi la wasanii wa Ilala almaarufu kama LAFamilia.[2] Benz anasifika sana kwa kupata ushirika mwingi kwa sasa kuliko msanii yeyote yule kwa Tanzania. Amewahi kushirikiana na Stara Thomas, Ray C., Lady Jay Dee, Tunda Man, Spark, Mwasiti, Mangwair, Maunda Zorro, na wengine wengi tu. Kwasasa Chid Benzi ni muathirika wa madawa ya kulevya,mwaka 2016 alipatiwa matibabu lakini akufanikiwa kumaliza tiba baada ya kutoka nyumba ya matibabu.

LA FAMILIA Ni kundi la msanii Chidi Benz kutoka ilala.Pia linahusishwa na vitendo vya kihalifu kama madawa ya kulevya na genge za kihuni(gangsta).

ILALA a.k.a iLA

Ni wilaya inayoongoza kwa uhalifu wa madawa ya kulevya,bangi,cocaine,heroin na wizi wa silaha. Mahali kama South Central Ilala ni hatari sana kwa vitendo hivyo.Maeneo mengine ni Yombo,Gongo la Mboto,Mchikichini,Jangwani,Kariakoo na Posta. Magenge mengi ya uhuni yameanzishwa Ilala. Kuna black gang,red gang na blues gang,hayo ndiyo yenye hamasa kubwa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Musical notes.svg Makala hii kuhusu muziki wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chid Benz kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.