Kitwechenkura
Kitwechenkura ni kata iliyomo ndani ya Wilaya ya Kyerwa, mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye msimbo wa posta namba 35823 [1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 16,106 [2]. Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, idadi ya wakazi wa kata ilikadiriwa kuwa watu 18,383.[3]
Jina la kata hiyo lilitokana na vichwa vya vifaru ambavyo miaka ya 1970 kulitokea operesheni ya vijiji vya ujamaa ambapo serikali iliwafukuza watu katika makazi yao wakahamia Kitwechenkura; walipofika lilikuwa pori kubwa, kazi yao ilikuwa kilimo na uwindaji walipokuwa wakiwaua vifaru vichwa vyao walivirundika pamoja.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tanzania Postcode List
- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 176
- ↑ Makadirio ya Idadi ya Watu katika Majimbo ya Uchaguzi kwa Mwaka 2016, Tanzania Bara, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dar es Salaam April 2016, iliangaliwa Mei 2021
Kata za Wilaya ya Kyerwa - Mkoa wa Kagera - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bugara | Bugomora | Businde | Isingiro | Iteera | Kaisho | Kakanja | Kamuli | Kibare | Kibingo | Kikukuru | Kimuli | Kitwe | Kitwechenkura | Kyerwa | Mabira | Murongo | Nkwenda | Nyakatuntu | Nyaruzumbura | Rukuraijo | Rutunguru | Rwabwere | Songambele |
|