Kisiwa cha Dubu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Bjornoya - Kisiwa cha Dubu.
Ramani ya Kisiwa cha Dubu.

Kisiwa cha Dubu (kwa Kinorwei: Bjørnøya byornoya; kwa Kiingereza: Bear Island) ni kisiwa kwenye mpaka wa magharibi ya Bahari ya Barents; au kwa lugha nyingine kiko takriban kwenye mpaka baina ya Bahari ya Aktiki na Atlantiki ya Kaskazini.

Hutazamwa kama kisiwa cha kusini kabisa cha funguvisiwa la Svalbard hata kama umbali wake na Spitsbergen ni km 235. Tangu mwaka 1920 kinahesabiwa kuwa sehemu ya Norwei.

Umbo la kisiwa linafana na pembetatu. Urefu toka kaskazini hadi kusini ni km 20, kutoka mashariki kwenda magharibi ni km 15.5. Eneo lote ni km² 178. Mwinuko wa juu ni mita 563 juu ya UB. Kwenye nusu ya kaskazini kuna maziwa mengi.

Kisiwa cha Dubu hakina wakazi wa kudumu, isipokuwa watumishi wachache wa kituo cha metorolojia cha Norwei. Nje ya kituo hicho kisiwa chote ni hifadhi ya mazingira.

Kuna miezi minne ambako jotoridi iko juu ya sentigredi sifuri.

Katika historia kisiwa hiki kilitembelewa mara kwa mara na wavuvi na mabaharia. Kwa vipindi tofauti kulikuwa na makazi ya wavuvi na wafanyakazi wa migodi lakini hayakudumu.

Jina la kisiwa kimetungwa na baharia Willem Barents aliyepita huko. Baada ya kuona dubu barafu kwenye bahari aliandika jina hilo kwenye ramani yake.

Makala hii kuhusu maeneo ya Norwei bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kisiwa cha Dubu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.