Kiongozi (ndege)
Kiongozi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Viongozi, vijumbe, walembe au ndege wa asali ni ndege wadogo wa familia Indicatoridae. Kwa kawaida jina “mlembe” hutumika kwa spishi za jenasi Prodotiscus na “kiongozi” kwa spishi nyingine. Ndege hawa wana rangi za kijivu, kahawa na nyeupe, pengine njano pia. Wabobea kwenye kula nta, kwa kawaida nta ya nyuki, lakini walembe na spishi ndogo za viongozi hula nta ya wadudu-gamba. Wanaitwa kiongozi kwa sababu spishi kadhaa (kiongozi mkubwa hasa) huongoza watu na wanyama kama nyegere mpaka masega ya nyuki. Watu au nyegere wakimaliza kutoa asali, kiongozi ala nta inayobaki. Viongozi hula majana, mafunza ya nta, wadudu wengine na buibui pia, na hata matunda mara kwa mara.
Viongozi hawatengenezi tago lao lenyewe. Jike hulitaga yai moja katika kila moja la matundu 5 au 6 ya spishi nyingine ya ndege, mara nyingi zile za vigong'ota, zuwakulu na goregore lakini walembe huchagua matago ya mviringo ya vinengenenge, videnenda, magamaga na vibwirosagi. Jike mmoja anaweza kuyataga mayai 20 katika mwaka mmoja. Domo la kinda la kiongozi lina kikulabu kinachotumika kwa kuyatoboa mayai ya mwenyeji na kuwaua makinda yake.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Indicator conirostris, Kiongozi Domo-nene (Thick-billed Honeyguide)
- Indicator exilis, Kiongozi-kuya (Least Honeyguide)
- Indicator indicator, Kiongozi Mkubwa (Greater Honeyguide)
- Indicator maculatus, Kiongozi Madoa (Spotted Honeyguide)
- Indicator meliphilus, Kiongozi-misitu (Pallid Honeyguide)
- Indicator minor, Kiongozi Mdogo (Lesser Honeyguide)
- Indicator pumilio, Kiongozi Kibete (Dwarf Honeyguide)
- Indicator variegatus, Kiongozi Mabaka (Scaly-throated Honeyguide)
- Indicator willcocksi, Kiongozi wa Willcocks (Willcocks's Honeyguide)
- Melichneutes robustus, Kiongozi Mkia-mpana (Lyre-tailed Honeyguide)
- Melignomon eisentrauti, Kiongozi Miguu-njano (Yellow-footed Honeyguide)
- Melignomon zenkeri, Kiongozi wa Zenker (Zenker's Honeyguide)
- Prodotiscus insignis, Mlembe Domo-jembamba (Cassin's Honeyguide)
- Prodotiscus regulus, Mlembe Mgongo-kahawia (Brown-backed au Wahlberg's Honeyguide)
- Prodotiscus zambesiae, Mlembe Mgongo-kijani (Green-backed Honeyguide)
Spishi za Asia
[hariri | hariri chanzo]- Indicator archipelagicus (Malaysian Honeyguide)
- Indicator xanthonotus (Yellow-rumped Honeyguide)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mlembe mgongo-kahawia