Kijiweni, Mvuleni
Kijiweni ni kijiji cha kata ya Mvuleni kilichopo katika Wilaya ya Lindi Vijijini, eneo ambalo mto Mbwemkuru unamwaga maji yake katika Bahari ya Hindi.
Kwa asili inasadikiwa hapa ndipo lilipotokea kabila la Wamachinga. Katika kipindi cha ukoloni palikuwa na mashamba makubwa ya mkonge yaliloitwa Mkoe, hali iliyosababisha pawepo na wageni wengi(wa makabila mbalimbali Kama wamakonde,wayaon.k) wengine wakiwa wamekuja kufanya kazi katika shamba la mkonge.
Mara nyingine kijiji hicho kinajulikana kama "Jiwe la Mzungu": hii ikiwa kutokana na alama ambayo iliwekwa na Wareno pwani ya Lindi katika kijiji hicho katika miaka ya karne ya 15. Inadaiwa kuwa Wareno (ambao waliweka jiwe hilo) walidai kuwa ndiyo sehemu ilipaswa uwe mpaka wao wa Kaskazini na himaya yao ya Msumbiji kwa mujibu wa Kikao cha Barlin.
Shughuli kuu za kiuchumi kwa wakazi wa Kijiweni ni kilimo cha mazao ya mtama, ufuta, korosho na mhogo. Shughuli nyingine kuu ni uvuvi hasa kwa vile kijiji kinapatikana kando ya bahari ya Hindi na mto Mbwemkuru.
Kijiweni kimebahatika kuwa na ufukwe mzuri wa bahari kiasi cha kuvutia wageni wengi. Kama ilivyo kwa vijiji vingi vya ukanda huo wa Mchinga, nyumba za wakazi wa Kijiweni zimepangwa kwa umahiri na ustadi wa hali ya juu kiasi cha kuweka muonekano mzuri wa mitaa yake Kama matimba,stendi,kizota,mjini majomani,mwela. Kijijini kuna zahanati na shule ya msingi, ghala la korosho,soko la Kijiji na ofisi ya mtendaji wa serikali ya kijiji.
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kijiweni, Mvuleni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |