Nenda kwa yaliyomo

Kentauro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya kuchongwa ya mapambano kati ya kentauro na binadamu (kutoka hekalu ya Parthenoni, Athini)
Kentauro anayepambana na wanyama witu (mozaiki katika Villa Hadriana karibu na Roma, iliumbwa mnamo mwaka 130 BK)

Kentauro (pia kantori, kantarusi) ni kiumbe cha hadithi za mitholojia ya Ugiriki ya Kale ambacho ni nusu farasi na nusu binadamu.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina lina asili katika Kigiriki κένταυρος kentauros, ila limekuwa centaurus kwa Kilatini na centaur kwa Kiingereza. Jina hilo liliingia katika Kiswahili kupitia Kiarabu قنطور qantur au قنطورس qantawrus. [1]

Mitholojia[hariri | hariri chanzo]

Kuna hadithi mbalimbali katika mitholojia ya Kigiriki kuhusu asili ya viumbe hao. Mojawapo ni kwamba walitokea baada ya kubakwa kwa pepo ya mawingu ya kike[2]. Nyingine ilisimulia jinsi gani mwanaume alizaa kentauro na farasi.

Wanahistoria wanahisi kwmaba asili ya hadithi hizo ilikuwa mshtuko wa watu ambao hawakutumia farasi walipokutana mara ya kwanza na wageni waliopanda farasi ilhali walishindwa kutofautisha mnyama na binadamu.[3]

Kentauro walitazamwa mara kama wapiganaji wakali, mara kama viumbe wenye hekima kubwa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Kentauro" ni umbo linalopendekezwa na kamusi ya KKK-ESD (2006), "kantarusi" ni jina la kundinyota lililorekodiwa na Knappert (1993), "kantori" ni umbo jinsi linavyotumiwa katika jina la nyota angavu zaidi ya kundinyota.
  2. Kentauroi, katika tovuti ya Theoi Greek Mythology, iliangaliwa Novemba 2020
  3. E.A. Lawrence, The Centaur: Its History and Meaning in Human Culture, jarida la Popular Culture, Volume27, Issue4, Spring 1994, Pages 57-68