Katerina Volpicelli
Mandhari
Katerina Volpicelli (aliishi Napoli nchini Italia 21 Januari 1839 - 28 Desemba 1894) alikuwa mwanamke tajiri wa mji huo ambaye maisha yake yote alihudumia maskini na wagonjwa. Kwa ajili hiyohiyo alianzisha shirika la masista "Wajakazi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu", ambamo alijitahidi daima ujitokeze upendo wa Kikristo katika mipango inayolingana na mahitaji ya jamii ya kisasa [1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Aprili 2001, halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu bikira tarehe 29 Aprili 2009[2].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Desemba kila mwaka[3][4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/90246
- ↑ Holy mass for the canonization of five new saints
- ↑ "Caterina Volpicelli (1839-1894)". www.vatican.va. Iliwekwa mnamo 2018-07-10.
- ↑ "Santa Caterina Volpicelli su santiebeati.it". Santiebeati.it. Iliwekwa mnamo 2018-07-10.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |