Kasiani wa Tanja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Marselo na Kasiani wa Tanja katika kanisa la Kiorthodoksi la Rabat, Moroko.

Kasiani wa Tanja alikuwa Mkristo wa Moroko aliyefia dini yake kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano. Tarehe inayotajwa na mapokeo ni 3 Desemba 298[1][2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Desemba[3][4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Geoffrey Ernest Maurice de Sainte-Croix, Christian Persecution, Martyrdom, and Orthodoxy, Oxford University Press, 2006, p. 172:"we must admit that we know nothing of the date or the circumstances of his execution"
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/80250
  3. Martyrologium Romanum
  4. https://catholicsaints.info/saint-cassian-of-tangiers/
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.