Kamera pembuzi

Kamera pembuzi (kwa Kiingereza: webcam) ni kifaa cha tarakilishi kinachotumika kwa kutoa video mtandaoni. Programu ya kamera pembuzi huwawezesha watumiaji kurekodi au kuonyesha video mubashara mtandaoni. Watu wanatumia kamera pembuzi kwa kuongea kama uso kwa uso mtandaoni baina ya watu wawili au zaidi, na maongezi hayo huweza kuwa ya sauti au video mubashara [1] .
Kamera pembuzi kwa kawaida huwa kamera ndogo kwa umbo ambazo huweza kuwekwa juu ya dawati au meza, au katika tarakilishi ya mtumiaji. Vipimo vya ukubwa wa kamera pembuzi huwa ni vidogo kuliko kamera nyingi za kubebwa mikononi, na udogo huo wa umbo hufanya kamera hizo kuwa za gharama ya chini ukilinganisha na kamera nyingi za kurekodi video, hata hivyo udogo huo bado huweza kukidhi maongezi ya video kwa urahisi.
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Miller, D., & Sinanan, J. (2014). Webcam. John Wiley & Sons.