Kakakuona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kakakuona
Kakakuona-nyika (Smutsia temminckii)
Kakakuona-nyika (Smutsia temminckii)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Pholidota (Wanyama waliopambika na magamba)
Familia: Manidae
Ngazi za chini

Jenasi 4:

Kakakuona ni wanyama wa familia Manidae ambao wamepambika na magamba na wana mkia mrefu. Wakitaka kujikinga dhidi ya wanyama mbuai wanajikunja.

Huishi katika kishimo cha kina cha hadi mita 3.5 au katika mti mvungu.

Hula mchwa na sisimizi na pengine wadudu wengine ambao huwakamata kwa ulimi wao mrefu wenye kunata.

Huzaa kidogo sana, na hiyo imechangia kufanya wapungue sana. Sababu nyingine ni ushirikina unaodai wanaleta bahati njema, hasa magamba yao. Ndiyo sababu nchini Tanzania wanalindwa na sheria kali hata wasikamatwe. Kakakuona-nyika anapatikana Hifadhi ya Serengeti.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]