Yohane Wall

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka John Wall)
Nje ya ukuta wa Harvington

John Wall, O.F.M. (Preston, 1620 - Worcester 22 Agosti 1679), alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo Warekoleti aliyefia dini ya Ukristo huko Uingereza, alipouawa kwa kunyongwa na kuchanwa utumbo baada ya kukamatwa wakati wa kuadhimisha Misa kwa siri kutokana na dhuluma ya mfalme Charles II.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini. Kwanza alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929, halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.