Nenda kwa yaliyomo

John Korir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

John Cheruiyot Korir (alizaliwa Disemba13, 1981) ni mwanariadha wa Kenya ambaye hujishughulisha na mbio za masafa Marefu. Anajulikana kwa sifa yake ya kungara katika majaribio lakini kushindwa katika mashindano makubwa[1].

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Korir alizaliwa katika mji wa Kiramwok, Wilaya ya Bomet nchini Kenya. alianza kukimbia akiwa katika shule ya Msingi. Alifuzu kutoka Shule ya Sekondari ya Merigi mnamo 1998. Hatimaye alisajiliwa na Kikosi cha Kenya Army mnamo 2001. Yeye ni wa kabila la Kipsigis, ambalo ni tabaka dogo la Kalenjin.

John Cheruiyot Kori na John Kipsang Korir

[hariri | hariri chanzo]

John Cheruiyot Korir anafaa kutofautishwa kutoka kwa John Kipsang Korir ambaye sana sana hushiriki katika mashindano ya Amerika. Wawili hawa wameshindana mara kadhaa. Katika mashindano ya Lisbon Half Marathon ya 2002, Kipsang Korir aliibuka bora, huku Cheruiyot akimshinda Kipsang katika shindano la Cross Country nchini Kenya mnamo 2003.

Katika shindano la Cherry Blossom 10-Mile Run la 2005, John Cheruiyot Korir aliibuka wa tano katika huku John Kipsang Korir akilishinda shindano hilo[2][3].

Meneja na Kocha

[hariri | hariri chanzo]

Meneja wake ni Gianni Demadonna, huku kocha wake akiwa Renato Canova.

Mafanikio

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Shindano Wenyeji Matokeo Vidokezo zaidi
2000 Mashindano ya Dunia ya Cross Country Vilamoura, Ureno 3 Chipukizi
Olympiki Sydney, Australia 5 Mita 10000
2001 Mashindano ya Dunia ya IAAF Cross Country Oostende, Ubelgiji 28 Masafa Marefu
Ubingwa wa Dunia Edmonton, Canada 8 10000m
2002 Michezo ya Majeshi ya Afrika Nairobi, Kenya Mshindi 10000m
Mashindano ya Jumuia ya Madola Manchester, Uingereza 4 10000m
Ubingwa wa Afrika Tunis, Tunisia 2 10000m
Mashindano ya Dunia ya Majeshi Mshindi 10000m
2003 Mashindano ya Dunia ya Cross Country Lausanne, Switzerland 6 Masafa marefu
Ubingwa wa Dunia Paris, Ufaransa 5 10000m
Mashindano ya Dunia ya Half Marathon Vilamoura, Ureno 4
2004 Mashindano ya Dunia ya Cross Country Brussels, Ubelgiji 11 Masafa Marefu
Olympiki Athens, Ugriki 6 10000m
Mashindano ya Dunia ya Half Marathon New Delhi, India 4
2005 Mashindano ya Dunia ya Cross Country Saint-Galmier, Ufaransa 9 Masafa Marefu
Ubingwa wa Afrika Bambous, Mauritius 4 10000m
2007 Mashindano ya Dunia ya Majeshi Hyderabad, India Mshindi 10000m
2008 Ubingwa wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia 4 10000m [4]

Matokeo ya Kujivunia

[hariri | hariri chanzo]

Uwanjani

Barabarani

  • Kilomita 10 27:49 (2005)
  • Kilomita 15 43:26 (2003)
  • Half marathon 1:00:47 (2004)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Virejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. IAAF, 1 Desemba 2006 John Cheruiyot Korir, the favourite in Lagos - PREVIEW Ilihifadhiwa 5 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
  2. Cherry Blossom: 28 Machi 2005: Two John Korirs Meet; Sally Barsosio Favorite in Women's Race Ilihifadhiwa 17 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
  3. "Cherry Blossom 10 Mile Road Race results 2005". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-04-17. Iliwekwa mnamo 2010-01-13.
  4. "Matokeo ya Addis Ababa 2008". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-03. Iliwekwa mnamo 2010-01-13.