Johann Paul Schor
Johann Paul Schor (1615 - 1674), anajulikana katika jiji la Roma kama "Giovanni Paolo Tedesco" (jina hili Tedesco kwa Kiitalia linamaanisha Mjerumani). Johann alikuwa msanii kutoka nchi ya Austria. Alikuwa mzalishaji wa michoro ya kupamba katika Baroque Roma, akichora michoro ya vitanda, milipuko ya mapambo ya fedha, nguo na hata vyakula vya sukari. Hapo zamani michoro yake mingi ilihusishwa na Gian Lorenzo Bernini.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa katika eneo la Innsbruck akiwa mwana wa familia kubwa ya wasanii wa Tyrol. Alipokea mafunzo kutoka studio ya baba yake, Hans Schor. Katika mwaka wa 1640 alijenga jina lake mjini Roma. Hapo, katika mwaka wa 1654, akawa mwanachama wa Accademia di San Luca, shule ya wasanii.
Akifuata mifano ya Bernini na Pietro da Cortona, uzuri wa michoro yake ulimpa umaarufu miongoni mwa wasanii na wapenzi wa sanaa. Hibbard (1958) aliandika: "aliunda kazi yake kwa njia ya kisanaa ya Cortona na Bernini kwa uhuru ulioonekana kutokana na Callot na Stefano Della Bella na wakati mwingine huonekana kushinda rococo".
Akiwa chini ya Cortona alisaidia katika kupamba Palazzo del Qirinale kwa ajili ya papa Alexander VII Chigi. Katika mwaka wa 1659, papa alimteua Schor kwa kazi ya kutumia michoro ya Bernini katika ujenzi wa kikanisa cha familia Chigi ('Capella Della Madonna del Voto katika Kanisa Kuu la Siena).
Akiwa Roma, Schor alimsaidia Bernini katika kuunda kifaa cha kukifunika Kiti Cha Mtakatifu Petro (Lanciani 1892) na katika kazi nyinginezo katika mwisho wa miaka ya 1650 na 1660. [1] Labda kazi yake maarufu kabisa ilikuwa baldacchino ya Santo Spirito huko Sassia.
Schor pia alisaidia kupamba vyumba vya Vatikano na vya Palazzo Borghese, aliposhirikiana na Carlo Rainaldi katika kupamba chemchemi ya nympheum iliyokuwa ikionyesha Venus akioga. Baadaye aliandaa michoro ya kupendekeza miundo mipya ya kupamba dari la Palazzo Colonna (1665-1668).
Upungufu wake kama msanii unaweza kuonekana kwa pambo alilounda mwaka 1650 la Musurgia Universalis ya Athanasius Kircher [2] lakini pambo hilo liliharibika kwa mipango mingi aliyotaka Kircher. Alipokuwa akifanya kazi pekee yake, michoro yake ilionyesha kazi bora zaidi.[3]
Katika studio yake katika miaka ya 1670 alimwajiri msanii wa Austria aliyekuwa kijana bado, Johann Bernhard Fischer. Fischer alirudi Vienna akafanya kazi yake hadi akapewa taji la Fischer Von Erlach, msanii maarufu wa asili ya Kivienna aliyefuzu katika miundo ya Baroque.
Johann Paulo Schor alikufa huko Roma katika mwaka wa 1674.
Watoto
[hariri | hariri chanzo]Wana wake Schor, Giovanni Paolo na Fillipo waliendeleza studio yake baada ya kifo chake. Wote wawili walikuwa miongoni mwa wasanii wa Roma waliopolekwa Napoli na kiongozi Gasparo de Haro y Guzman, marqués del Carpio katika mwaka wa 1683. Miongoni mwa wanamuziki wa kiongozi huyo alikuwa Alessandro Scarlatti. Del Carpio alikutana na wasanii hao kwa kupitia mwana wa mfalme Lorenzo Onofrio Colonna, aliyekuwa mwanajeshi wa Napoli ilhali del Caprio alikuwa balozi wa Hispania. [4] Katika mwaka wa 1690,Cristofor Schor alifanya mabadiliko madogo kwa muundo wa Martino Longhi wa Sant'Antonio dei Portoghesi. Johann Ferdinand Schor alikuwa msaidizi wa studio wa Carlo Maratta.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]- ^ Howard Hibbard, "Palazzo Borghese Studies I: The Garden and its Fountains" Gazeti la Burlington 100 No. 663 (Juni 1958, pp. 204–212)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Stefanie Walker, tuzo ya Roma kwa kusoma juu ya Schor Ilihifadhiwa 21 Desemba 2005 kwenye Wayback Machine..