Jeshi la Anga la Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Jeshi la Anga la Kenya ni tawi la Majeshi ya Ulinzi ya Kenya kwa ajili ya vita vya hewani.

Moi Air Base, Eastleigh ndio makao makuu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jeshi la Anga la Kenya liliundwa tarehe 1 Juni 1964, baada ya uhuru kwa msaada wa Uingereza.[1]

Lilivunjwa baada ya mapinduzi yaliyoshindikana kufanywa na maafisa wa jeshi hili tarehe 1 Agosti 1982. Shughuli zake zilianzishwa tena na kudhibitiwa vikali chini ya jeshi lililojulikana kama 82 Air Force. Jeshi la Anga lilipata uhuru wake tena mwaka 1994.

Tarehe 10 Aprili 2006 ndege KAF Harbin Y-12 ilianguka karibu na Marsabit ikiwa na abiria 17, na kati yao 14 walikufa. Ndani, mlikuwemo wanasiasa; Bonaya Godana, waziri wa zamani, alikuwa miongoni mwa majeruhi. Nahodha alikuwa Meja David Njoroge.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "It’s a Golden Jubilee for Kenya Air Force!", Wizara ya Ulinzi, Ilipatikana mnamo 2018-03-18