Jerlando wa Agrigento

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Jerlando wa Agrigento (au Gerland wa Besançon (alifariki 25 Februari 1100) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki huko Agrigento, Sicilia, leo nchini Italia.

Alitangazwa mtakatifu mwaka 1159. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Februari.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Inasadikika kwamba alizaliwa Besançon (Ufaransa), akiwa ndugu wa mfalme wa Kinormani Roger I wa Sisilia.

Baada ya huyo kufukuza Waarabu kutoka kisiwa cha Sisilia, mwaka 1088 (au 1093) alimuita Jerlando awe askofu wa kwanza wa Agrigento baada ya utawala wa Kiislamu, ili arudishe Ukristo katika kisiwa chote.

Alifanya kazi hiyo kwa bidii na mafanikio hadi kifo chake

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jerlando wa Agrigento kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.