Jenerali Ulimwengu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jenerali Twaha Ulimwengu (alizaliwa 4 Aprili 1948 katika wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera [1] nchini Tanzania) ni mwanahabari na mwanasheria ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi katika gazeti la Raia Mwema la jijini Dar es Salaam nchini Tanzania [2]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Jenerali alisoma katika shule ya Kamachumu na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki (University of East Africa) aliposoma sheria kati ya mwaka 1969 na 1972.

Utumishi wa TANU na serikali[hariri | hariri chanzo]

Baada ya masomo aliajiriwa na gazeti la Daily News kati ya miaka 1972 hadi 1974. Mwaka huo alitumwa kwenda Aljeria kama mwakilishi wa Tanzania kwenye ofisi kuu ya Harakati ya Vijana wa Afrika (Panafrican Youth Movement) alipokaa hadi 1985.

Aliporudi alipewa nafasi kati Umoja wa Vijana wa TANU. Mwaka 1987 alikuwa mkurugenzi wa vijana na michezo katika Wizara ya Vijana na Michezo.

Mwaka 1989 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Ilala, na mwaka 1990 aliteuliwa katika bunge la taifa hadi 1995.

Mjasiriamali wa habari[hariri | hariri chanzo]

Wakati alipokuwa mbunge, aliunda shirika la Habari Corporation akaanzisha gazeti la Rai, iliyofuatwa na magazeti ya Mtanzania na The African.

Michango yake magazetini, pamoja na ukosoaji wa wanasiasa mbalimbali, ilisababisha hatua ya serikali ya rais Mkapa ya kufuta uraia wake kwenye Februari 2001. Akiambiwa aombe kukubaliwa alikataliwa mara moja mwaka 2002 halafu akakubaliwa tarehe 11 Machi 2004[3].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]