Isidori wa Pelusio
Isidori wa Pelusio (kwa Kigiriki: Ἰσίδωρος ὁ Πηλουσιώτης; alifariki 450 hivi) alikuwa mmonaki padri wa Misri.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Februari[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Mtoto pekee wa familia maarufu wa Aleksandria[2], akiwa ameshajipatia ujuzi mwingi, alitawa kwenye mlima karibu na mji wa Pelusium, kwa kufuata nyayo za Yohane Mbatizaji na Mababu wa jangwani.
Pia alijitosa kuhubiri kwa mfano wa Yohane Krisostomo akamtetea dhidi ya dhuluma kutoka kwa patriarki Theofilo wa Aleksandria, ndugu yake, na kwa malkia Eudosia.
Maandishi
[hariri | hariri chanzo]Anajulikana kwa barua 2,000 hivi alizowaandikia patriarki Sirili wa Aleksandria, kaisari Theodosius II na wengineo wengi.[3] Baadhi yake ni muhimu kwa ufafanuzi wa Biblia.[4]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ "Venerable Isidore of Pelusium". oca.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-03-17.
- ↑ Pierre Evieux, Isidore de Peluse, 1995. A study of the man and his works, in French.
- ↑ C.H.Turner, The letters of Isidore of Pelusium, Journal of Theological Studies 6 (1905)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Coptic Encyclopedia entry for Isidorus of Pelusium
- A few letters in English translation
- Isidore of Pelusium and the holy scriptures (in Greek) by EIRINI ARTEMI
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |