Nenda kwa yaliyomo

Inosenti wa Imakulata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Inosenti akiwa amevaa kanzu ya shirika lake.

Inosenti wa Imakulata, C.P. (jina la kuzaliwa: Manuel Canoura Arnau; Foz, Lugo, 10 Machi 1887Turon, 9 Oktoba 1934) alikuwa padri Mpasionisti wa Hispania[1] aliyeuawa na waasi wa dini bila kesi kwa ajili ya imani yake, akiwa pamoja na mabradha 8 wa shirika la Mabradha wa Shule za Kikristo: Sirili Bertran, Marchano Yosefu, Viktoriano Pio, Benjamini Juliani, Juliani Alfredo, Augusto Andrea, Benito wa Yesu na Aniseto Adolfo[2][3].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 19 Aprili 1990, halafu mtakatifu tarehe 21 Novemba 1999 pamoja na wafiadini wenzake.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.