Aniseto Adolfo
Mandhari
Aniseto Adolfo (Celada Marlantes, Santander, Oktoba 1912 - Turon, 9 Oktoba 1934) alikuwa bradha wa Kanisa Katoliki na mlezi wa vijana katika shirika la Mabradha wa Shule za Kikristo[1].
Aliuawa kwa imani yake pamoja na wenzake 7 (Sirili Bertran, Marchano Yosefu, Viktoriano Pio, Benjamini Juliani, Juliani Alfredo, Augusto Andrea na Benito wa Yesu[2][3]) na padri Mpasionisti Inosenti wa Imakulata wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Aprili 1990, halafu mtakatifu tarehe 21 Novemba 1999.
Sikukuu inaadhimishwa tarehe ya kifodini chake[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/100140
- ↑ Cirilo Bertrán and 8 Companions, religious of the Institute of Brothers of the Christian Schools and Inocencio de la Inmaculada, priest of the Congregation of the Passion of Jesus Christ, martyrs (+1934, +1937)
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/91625
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |