"I Have Nothing" ni jina la wimbo ulioimbwa na mwimbaji maarufu kutoka nchini Marekani - hayati Whitney Houston. Wimbo ulitolewa ukiwa kama single kutoka katika albamu ya kibwagizo cha filamu The Bodyguard: Original Soundtrack Album (1992) mnamo tarehe 20 Februari, 1993, kupitia studio za Arista Records. Wimbo ulitungwa na David Foster na Linda Thompson, na kutayarishwa na Foster. Wimbo huu umejawa na midundo mikali ya balad linalozungumzia mikasa inayowatokea wapendanao katika suala zima la kutunzana na kujaliana.
Baada ya mafanikio yake katika "I Will Always Love You" na "I'm Every Woman," "I Have Nothing" bado ukaendelea kuwa wimbo bab-kubwa, kwa kushika nafasi ya nne kwenye chati za Billboard Hot 100 na kutunukiwa Dhahabu na Recording Industry Association of America. Wimbo huu pia ukaja kuwa mkali kwenye chati za Billboard Hot R&B Singles, ukiwa pia nafasi ya nne, na nafasi ya kwanza kwenye Billboard Adult Contemporary. Mfanikio haya yalimfanya Houston kuwa msanii wa kwanza katika historia nzima ya chati za Billboard kuwa na nyimbo tatu katika wiki za awali kabisa huku vibao vyote vikiwa vinatoka katika albamu za vibwagizo vya filamu kwa mwaka huo wa 1991.
↑"Whitney Houston". Wweb.uta.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-06-26. Iliwekwa mnamo 2017-01-30.
↑"I have nothing". Wweb.uta.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-25. Iliwekwa mnamo 2017-01-30.
↑"The RPM Top 100 Hit Tracks of 1993". RPM. 58 (23). RPM Music Publications Ltd. Desemba 18, 1993. ISSN0315-5994. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-21. Iliwekwa mnamo Machi 12, 2011. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)