Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa, Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa (kwa Kiingereza: National Intelligence Service, kifupi: NIS) ni shirika la upelelezi ndani na nje mwa Kenya ili kuhakikisha usalama wa nchi. Asili yake ilikuwa Tawi Maalum (kwa Kiingereza: Special Branch, kifupi: SB) iliyokuwa idara ya polisi kutoka mwaka 1952 hadi mwaka 1999 kama Idara ya Ujasusi.[1] 

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tawi Maalum (SB)[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1926, Idara ya Uchunguzi wa Jinai iliundwa na wakoloni na kuwa na tawi lenye jukumu la upelelezi. Kati ya Vita vikuu vya pili vya dunia hadi mwaka 1963, shughuli za SB zilijumuisha upelelezi wa wananchi waliokuwa wakidai uhuru, vuguvugu la vyama vya wafanyakazi na Mau Mau.

Serikali za nyakati za baada ya uhuru zilitumia SB kukandamiza wapinzani. Mwaka 1998, Huduma ya Ujasusi wa Usalama wa Kitaifa (kwa Kiingereza: National Security Intelligence Service, kifupi: NSIS) ilibuniwa na zaidi ya maafisa 170 kupigwa kalamu. Katika mwaka 1999, NSIS na Huduma ya Polisi zilitenganishwa, mamlaka ya NSIS ya kukamata washukiwa kuondolewa, na mahakama kuanzishwa ili isikize malalamiko dhidi ya SB.

Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa[hariri | hariri chanzo]

NIS iliundwa upya na Katiba ya Kenya ya Mwaka 2010. Inaongozwa na Sheria ya Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa ya mwaka 2012.

Majukumu[hariri | hariri chanzo]

  • Kuchunguza na kutambua tishio lolote kwa Kenya
  • Kutoa ushauri kwa Rais na Serikali kuhusu tishio lolote kwa usalama wa Kenya
  • Kuchukua hatua za kulinda maslahi ya kiusalama ya Kenya yawe upande wa siasa, jeshi au uchumi
  • Kuchuja watu watakaoshikilia nafasi inayohitaji kibali cha usalama.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. NSIS Historical Background. National Security Intelligence Service (2006). Jalada kutoka ya awali juu ya 22 December 2007.