Idara ya Uchunguzi wa Jinai, Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Idara ya Uchunguzi wa Jinai (kwa Kiingereza: Directorate of Criminal Investigations, kifupi: DCI au CID) ni kitengo cha Huduma ya Polisi ya Kenya ambacho jukumu lake kuu ni uchunguzi wa jinai. Inaongozwa na Mkurugenzi ambaye huteuliwa na Rais na kuripoti kwa Mkaguzi Mkuu wa Polisi. Makao makuu yako katika Barabara ya Kiambu, Nairobi.

Vitengo[hariri | hariri chanzo]

DCI ina vitengo vifuatavyo[1]:

  • Kitengo cha Uchunguzi
  • Kitengo cha Utendakazi
  • Kitengo cha Sheria na Masuala ya Jinai
  • Chuo cha DCI
  • Vitengo vyenye kazi maalum
  • Kitengo cha Utawala

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Organogram", Idara ya Uchunguzi wa Jinai, Ilipatikana mnamo 2018-03-18