Historia ya Intaneti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Intaneti (kutoka Kiingereza "Internet") ni mfumo mkubwa ambao mamilioni ya kompyuta na mifumo na uendeshaji wa mfumo wa aina zote yanaweza kuwaunganisha. Hii ina maana ya mahusiano ya dunia yote pamoja.

Historia yake inaweza kuanza na uzinduzi wa Sputnik na USSR uliochochea Marekani kuanzisha shirika la utafiti wa juu wa miradi, iliyojulikana kama ARPA, katika mwezi Februari 1958 ili kuongoza kiteknolojia.[1] [2] ARPA ilitengeneza ofisi ya teknolojia za kuchambua habari (IPTO) ili kuendeleza utafiti wa programu inayojitekeleza ya mazingira ya chini (Sage), ambayo iliunganisha mifumo ya rada za nchi nzima kwa mara ya kwanza.

J. C. R Licklider alichaguliwa kuwa kiongozi wa IPTO. Licklider alihama kutoka maabara ya masomo yanayochunguza jinsi ubongo wa binadamu unavyofasiri sauti katika Chuo Kikuu cha Harvard MIT mwaka 1950, baada ya kuvutiwa na teknolojia ya habari. Akiwa MIT, alikuwa kwenye kamati iliyoanzisha Maabara ya Lincoln na kufanya kazi ya mradi wa Sage. Mwaka wa 1957 akawa makamu wa rais katika BBN, ambapo alinunua kompyuta ya kwanza ya PDP-1 na kuongoza maonyesho ya kwanza ya ugawanaji muda.

Akiwa IPTO, Licklider alimleta Lawrence Roberts ili aanzishe mradi wa kutengeneza mtandao, na Roberts alikita msingi wa teknolojia katika kazi ya Paulo Baran, [3] ambaye alikuwa ameandika masomo kamili kwa Wanajeshi wa waangani wa Marekani akipendekeza ubadilishaji pakiti (badala ya ubadilishaji mzunguko) ili kupata mtandao bora unaobadilika na unaoweza KUstahimili janga. Profesa wa UCLA Leonard Kleinrock alikuwa ametoa msingi wa nadharia ya pakiti za mitandao mwaka 1962, na baadaye, katika mwaka 1970, wa upitishaji wa kiviwango, dhana ambazo zimekuwa msingi wa maendeleo ya intaneti ya leo.

Baada ya kazi nyingi, sehemu mbili za kwanza ambazo zingekuwa ARPANET ziliunganishwa kati ya Shule ya Uhandisi na Sayansi Tumikizi ya UCLA na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti ya Stanford (SRI) katika bustani ya Menlo, California, tarehe 29 Oktoba 1969. ARPANET ilikuwa moja ya mitandao tangulizi ya mtandao wa intaneti ya leo. Kufuatia maonyesho kuwa ubadilishaji pakiti ulifanya kazi kwa ARPANET, kituo cha posta cha Uingereza, Telenet, TRANSPAC na DATAPAC zilishirikiana kuunda mtandao wa kwanza wa huduma ya ubadilishaji pakiti. Nchini Uingereza, hii ilikuwa inajulikana kama huduma ya kimataifa ya ubadilishaji pakiti (IPSS), mwaka 1978. Mkusanyiko wa mitandao yenye msingi wa X.25 ilikua kutoka Ulaya na Marekani na kutanda Kanada, Hong Kong na Australia kufikia mwaka 1981. Sheria ya ubadilishaji pakiti ya X.25 ilitengenezwa katika CCITT (sasa inaitwa ITU-T) mwaka 1976.

X.25 ilikuwa huru kutoka itifaki ya TCP/IP ambayo iliinuka kutokana na kuwa kazi ya majaribio ya DARPA kwenye ARPANET, mtandao wa Pakiti za Redio na Mtandao wa Pakiti ya Setilaiti wakati mmoja. Vinton Cerf na Robert Kahn walitengeneza maelezo ya kwanza ya itifaki ya TCP mwaka 1973 na kuchapisha karatasi kuhusu mada hii katika mwezi Mei 1974.

Matumizi ya neno "Internet" kuelezea mtandao mmoja wa kiulimwengu wa TCP/IP yalianza katika mwezi Desemba 1974 na uchapishaji wa RFC 675, yakiwa maelezo kamili ya kwanza ya TCP iliyoandikwa na Vinton Cerf, Yogen Dalal na Carl Sunshine, waliokuwa katika Chuo Kikuu cha Stanford. Katika miaka tisa iliyofuata, kazi iliendelea kurekebisha itifaki hizo na kuzitekeleza katika mifumo ya oparesheni ya aina mbalimbali. Mtandao wa Kwanza wenye upana mkubwa wa msingi wa TCP / IP ulikuwa ukifanya kazi kufikia tarehe 1 Januari 1983 wakati ambapo viwekaji vyote vya ARPANET vilibadilishwa kutoka itifaki za hapo awali za NCP. Mwaka 1985, Wakfu wa Sayansi wa kitaifa Marekani (NSF) uliamuru ujenzi wa NSFNET, uti wa mgongo wa mtandao wa chuo kikuu wenye kasi ya kilobaiti 56 kwa sekunde kwa kutumia kompyuta zilizoitwa "fuzzballs" na mvumbuzi wake, David L. Mills. Mwaka uliofuata, NSF ilifadhili ubadilishaji hadi mtandao wenye kasi ya juu zaidi ya megabaiti 1.5 kwa sekunde. Maamuzi muhimu kutumia itifaki za DARPA TCP/IP ulifanywa na Dennis Jennings, aliyekuwa msimamizi wa programu ya kompyuta zenye nguvu huko NSF.

Ufunguzi wa mtandao huo kwa maslahi ya kibiashara ulianza mwaka wa 1988. Baraza ya Mitandao ya Kimajimbo Marekani ilikubali ushikanishaji wa NSFNET na mfumo wa barua wa MCI katika mwaka huo, kiungo kilifanywa katika msimu wa joto wa mwaka wa 1989. Huduma zingine za kielektroniki za kibiashara zilishikanishwa zikiwemo: OnTyme, Telemail na Compuserve. Katika mwaka huo, watoaji wa huduma ya Intanet watatu waliundwa: UUNET, PSINet na CERFNET. Muhimu, mitandao tofauti iliyotoa viingilio, na baadaye kuungana na Intanet ilikuwa BITNET na Usenet. Mitandao mingine ya kibiashara na elimu kama Telenet, Tymnet, Compuserve na JANET iliunganishwa na Intanet iliyokuwa ikikua. Telenet (iliyoitwa Sprintnet baadaye ) ulikuwa mtandao mkubwa wa kompyuta wa kitaifa uliofadhiliwa kibinafsi, wenye upigaji simu ya intaneti burekatika miji, kote Marekani na uliyokuwa ukifanya kazi tangu mwongo wa 1970. Hatimaye, mtandao huu uliunganishwa na mingine katika mwongo wa 1980 wakati ambapo itifaki ya TCP / IP iliendelea kuwa maarufu zaidi. Uwezo wa TCP/IP kufanya kazi kwa karibu mtandao wowote wa mawasiliano uliruhusu ukuaji rahisi, ingawa ukuaji wa haraka wa Intanet ulikuwa juu ya upatikanaji rahisi wa safu ya vielekezi vya kibiashara kutoka makampuni mengi, upatikanaji wa vifaa vya kibiashara vya Ethanet ya mitandao ya mitaa, na kuenea kwa utekelezaji na uwekaji sheria mkali wa TCP / IP katika UNIX na karibu kila mfumo mwingine wa oparesheni.

Ingawa vifaa msingi na miongozo vinavyofanya uwezekanaji wa intanet vimekuwepo kwa karibu miongo miwili, mtandao huo haukupata kuona nyuso za umma mpaka mwongo wa 1990. Tarehe 6 Agosti 1991, CERN, shirika ya Ulaya ya utafiti wa chembe, ulieleza umma kuhusu mradi mpya wa matandao wa dunia nzima. Mtandao ulizuliwa na mwanasayansi waKiingereza Tim Berners-Lee mwaka wa 1989. Kivinjari cha mtandao kilichokuwa cha kwanza na chenye umaarufu sana kilikuwa ViolaWWW, iliyofuata mtindo wa HyperCard na kujengwa kwa kutumia mfumo wa X Window. Hatimaye ilichujwa na umaarufu wa tovuti ya Mosaic. Mwaka wa 1993, Kikao kikuu cha zana za kompyuta zenye nguvu katika Chuo Kikuu cha Illinois ilitoa aina ya kwanza 1.0 ya Mosaic, na mwisho wa mwaka wa 1994 hamu ya umma iliongezeka Intanet ambayo hapo awali ilikua ya taaluma na ufundi. Kufikia mwaka 1996 matumizi ya neno Intaneti yalikuwa kawaida, na kwa hiyo, hata matumizi yake kama kisawe cha mtandao wa ulimwengu mzima.

Muongo huo ulipoendelea, intaneti ilifanikiwa kushughulikia mitandao mingi binafsi wa awali (ingawa baadhi ya mitandao, kama FidoNet, vimebaki tofauti). Katika miaka ya 1990, ilikuwa inakadiriwa kwamba intaneti ilikua kwa asilimia 100 kila mwaka, na kipindi kifupi cha mwaka wa 1996 na 1997 ukuaji wake ulilipuka. [4] Ukuaji huo ulitokana na ukosefu wa utawala mkuu, ambao unaruhusu ukuaji wa kikaboni wa mtandao, na pia ukosaji ubinafsi na huru katika itifaki za intaneti, ambao unahamasisha ubadilishaji wauzaji na kuzuia kampuni yoyote kuwa na udhibiti mkubwa wa mtandao. [5] Makadirio ya idadi ya watumiaji wa internet ni bilioni 1.67 kufikai 30 Juni 2009. [6]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. ARPA/DARPA. Defense Advanced Research Projects Agency. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-04-07. Iliwekwa mnamo 2007-05-21.
  2. DARPA Over the Years. Defense Advanced Research Projects Agency. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-04-07. Iliwekwa mnamo 2007-05-21.
  3. Baran, Paul (1964). On Distributed Communications. 
  4. Coffman, K. G; Odlyzko, A. M. (1998-10-02). "The size and growth rate of the Internet" (PDF). AT&T Labs. Retrieved 2007-05-21. 
  5. Comer, Douglas (2006). The Internet book. Prentice Hall. p. 64. ISBN 0132335530. 
  6. World Internet Users and Population Stats. Internet World Stats. Miniwatts Marketing Group (2009-06-30). Iliwekwa mnamo 2009-11-06.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Intaneti kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.