Nenda kwa yaliyomo

Kihindustani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hindi-Urdu)
Neno "Hindustani" kwa maandishi ya Devanagari na Kiarabu.
Uenezi wa Kihindustani.

Kihindustani (pia: Kihindi-Kiurdu) ni lugha ya pamoja kaskazini mwa Uhindi na Pakistan. Inapatikana kwa umbo sanifu tofauti katika nchi hizo: Kihindi katika India na Kiurdu katika Pakistan.

Kinahesabiwa kuwa kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi ndani ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Lugha za karibu ni pamoja na Kipunjabi, Kisindhi, Kigujarati, Kimarathi na Kibengali.

Mwandiko ni tofauti kila nchi, yaani upande wa Pakistan inaandikwa kwa herufi za Kiarabu na upande wa Uhindi kwa herufi za Devanagari. Lakini kama lugha ya majadiliano hakuna tofauti. Sarufi ni sawa, ila kuna kiasi cha tofauti katika msamiati hasa, katika lugha ya maandishi. Upande wa Kiurdu / Pakistan kuna maneno mengi zaidi yenye asili ya Kiarabu, Kituruki na Kiajemi. Upande wa Uhindi waandishi hutumia zaidi maneno yenye asili ya Kisanskrit.

Kabla ya ugawaji wa Uhindi ya Kiingereza mwaka 1947 majina kama Hindustani, Urdu, na Hindi yalikuwa na maana ileile na kutumiwa kwa mchanganyiko. Leo hii neno "Hindustani" bado hutumiwa kwa lugha inayozungumzwa kote Uhindi kaskazini na Pakistan, pia mara nyingi kwa ajili ya lugha ya Wahindi wanaokaa nje ya Uhindi tangu muda mrefu kwa mfano: Kihindi cha Fiji na Kihindustani cha Surinam.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]