Nenda kwa yaliyomo

Heli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Helium)


Heli
Jina la Elementi Heli
Alama He
Namba atomia 2
Mfululizo safu Gesi adimu
Uzani atomia 4.002602
Valensi 2
Densiti 0.1785 kg/m3
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka - K (-272.2 °C)
Kiwango cha kuchemka 4.22 K (-268.93 °C)
Hali maada gesi

Heli (pia heliamu, ing. helium; kut. kigiriki ἥλιος hélios "jua") ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 2 na uzani wa atomi 4.002602. Alama yake ni He. Ni atomi nyepesi ya pili kati ya elementi zote hivyo ina nafasi ya pili katika mfumo radidia wa elementi.

Laser ya Heli

Huhesabiwa kati ya gesi adimu kwa sababu haimenyuki na elementi nyingine. Heli iko katika hali ya gesi hata kama halijoto au baridi ni kali ikiganda karibu na sifuri halisi tu; ni elementi ya pekee isiyoganda kabisa hata kwenye sifuri halisi kama shindikizo ni la kawaida.


Muundo wa atomi

[hariri | hariri chanzo]

Atomi za He hutokea mara nyingi yenye kiini cha protoni mbili na nyutroni mbili kinachozungukwa na elektroni mbili katika ganda moja lilele. Hali hii ya kawaida huitwa isotopi ya 4He .

Heli haliathiri au kuathiriwa kirahisi hivyo gesi yake haina herufu au ladha. Hupatikana kwa umbo la atomi tu maana haiingii katika molekyuli.

Upatikanaji

[hariri | hariri chanzo]

Ulimwenguni kote heli ni elementi inayopatikana kwa wingi, Kutokana na nadharia ya mlipuko mkuu unakadiriwa kuwa na asilimia 25 ya masi yote ya ulimwengu.

Ndani ya Jua letu heli inaundwa kwa wingi ilhali hidrojeni huunganika kinyuklia kuwa heli na machakato huu unatokea katika nyota nyingi.

Hapa duniani petu ni elementi haba. Katika angahewa ya dunia heli ina kiwango cha asilimia 0.00052 % au 5.2 ppm. Heli ni gesi nyepesi kuliko oksijeni na nitrojeni ya hewa na hivyo inapanda juu ndani ya angahewa na kupotea muda wote kuelekea angani.

Hutokea pia katika miamba ya ganda la dunia katika mbunguo nururifu wa urani katika ardhi. Heli inayotokea hapa inapanda juu polepole na kuingia katika angahewa. Pale ambako kuna maganda ya mwamba usiopitika na gesi, heli inakusanyika, kwa kawaida pamoja na gesi asilia nyingine.

Hivyo heli inatolewa pale inapopatikana ndani ya gesi ya asilia wakati wa kutoa gesi hii. Kiwango cha heli ndani ya gesi asilia ni kuanzia ppm chahce hadi kufikia asilimia 7-10.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Heli inatumiwa katika teknolojia mbalimbali hasa pale ambako baridi kali huhitajiwa kwa sababu haigandi. Tabia yake ya kutoathiriana na elementi nyingine imeifanya kuwa gesi salama kwa ajili ya chomboanga.