Nenda kwa yaliyomo

Ugonjwa wa moyo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Heart disease)
Moyo wa binadamu.

Ugonjwa wa moyo ni maradhi yanayoushambulia na kuudhoofisha moyo. Moyo ni kiungo kinachosukuma damu katika mwili wa kiumbe hai, hasa wanyama. Damu hiyo huwa na vitu kama oksijeni, homoni, seli za damu na virutubishi mbalimbali kutoka katika vyakula anavyokula. Ugonjwa wa moyo mara nyingi huwapata binadamu kuliko wanyama wengine.

Visababishi vya ugonjwa

[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa wa moyo huweza husababishwa na tabia au namna mtu anavyoishi, magonjwa mbalimbali pamoja na aina ya chakula anachokula mtu huyo. Kwa upande wa tabia mtu anaweza kupata ugonjwa wa moyo kupitia unywaji pombe kupita kiasi, uvutaji wa sigara na uvivu wa kufanya mazoezi. Mazoezi humsaidia mtu awe mwenye afya kwani mazoezi hudhoofisha viini vya magonjwa mbalimbali vilivyo ndani ya mwili wa binadamu.

Ugonjwa wa moyo pia husababishwa na matatizo katika mlo wa mtu, hasa katika kuzidisha (kuongeza) viwango vinavyohitajika na mwili. Kuzidisha viwango vya chakula ni kama kula vyakula vyenye mafuta mengi ambapo mafuta hayo huweza kujaa mwilini hata mpaka kwenye moyo na kusababisha kuziba kwa mshipa wa damu hivyo kufanya moyo ushindwe kufanya kazi vizuri.

Magonjwa ambayo huweza kuuathiri moyo ni kama ugonjwa wa kisukari pamoja na shinikizo la damu. Ugonjwa wa kisukari husababishwa na mwili kushindwa kuongoza kiwango cha sukari katika damu. Shinikizo la damu pia huchangia kupelekea kwa ugonjwa wa moyo kwani huasababisha mshipa mbalimbali ndani ya moyo kuweza kupasuka.

Tahadhari

[hariri | hariri chanzo]

Ili kuepukana na ugonjwa wa moyo binadamu anashauriwa kwanza ale mlo kamili, afanye mazoezi angalau mara moja au mbili kila siku, kujiepusha na unywaji wa pombe na vilevi vingine pamoja na uvutaji wa sigara ambao husababisha hata magonjwa ya mapafu pia kuepuka kutumia vyakula venye kiasi kikubwa cha mafuta na sukari. Mwanadamu pia anashauriwa apate tiba iliyo kamili pale anapogundulika kuwa na magonjwa makubwa, hasa kisukari na shinikizo kubwa la damu. Pia inashauria mtu kufanya uchunguzi (check up) mara kwa mara ili kuweza kujua afya yake inavyoendelea: hii itamsaidia kuyajua na kuyawahi magonjwa kabla hayajawa makubwa.

Ugonjwa wa moyo husababisha kifo kwani moyo ndio kiungo kikuu cha kusukuma damu, hivyo kinaposhindwa kufanya kazi hupelekea mwisho wa maisha ya kiumbe hai huyo.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugonjwa wa moyo kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.