Gorée

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya kale ya kisiwa(1772)
Gorée
Gorée inavyoonekana kutoka baharini
Gereza la watumwa


Gorée (kifaransa: Île de Gorée) ni kisiwa cha Atlantiki mbele ya pwani la Senegal na sehemu ya manisipaa ya Dakar. Ilijulikana kama kituo cha biashara ya watumwa. Hadi kukomeshwa kwa biashara hiyo mwaka 1848 watumwa walipelekwa kisiwani kutoka bara, kufungwa katika majela, kuuzwa kwenye minada na kubebwa Amerika kwa jahazi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa kina urefu wa 1000 m na upana wa 300m, eneo lake ni 36 ha.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa kiliingia chini ya utawala wa Ureno mwaka 1444 BK. Uholanzi ilivamia Goree mwaka 1588. Katika karne zilizofuata Ufaransa na Uingereza zilishindana juu ya utawala wa kisiwa. Tangu 1815 kilikuwa chini ya Ufaransa. Mwaka 1879 idadi ya wakazi ilikuwa 2,956 (Wazungu 50, Chotara 750 na wengine Waafrika).

Makumbusho ya Gereza la Watumwa yamekuwa mahali pa utalii. Waamerika weusi walianza kufika kisiwani kutafuta nyayo za mamabu waliobebwa kutoka hapa kama watumwa wafungwa.

Mwaka wa 1978, kisiwa cha Goree kiliingizwa na UNESCO katika orodha la Urithi wa Dunia.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons