Nenda kwa yaliyomo

Mbung'o

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Glossina)
Mbung'o
Mbung'o-nyika (Glossina sp.)
Mbung'o-nyika (Glossina sp.)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Diptera (Wadudu wenye mabawa mawili tu)
Nusuoda: Brachycera (Diptera wenye vipapasio vifupi)
Zetterstedt, 1842
Familia ya juu: Hippoboscoidea
Familia: Glossinidae
Jenasi: Glossina
Wiedemann, 1830
Ngazi za chini

Nusujenasi 3 na spishi 22:

Msambao wa mbung'o
Msambao wa mbung'o

Mbung'o, chafuo au ndorobo ni nzi wa jenasi Glossina, jenasi pekee ya familia Glossinidae katika oda Diptera ambao wanafyonza damu ya mamalia pamoja na watu. Wanaenezea watu ugonjwa wa malale na wanyama nagana, yanayosababishwa na vijidudu wa jenasi Trypanosoma. Nzi hao hutokea Afrika tu (angalia ramani).

Chakula cha mbung'o ni damu ya mamalia hasa. Spishi fulani hufyonza damu ya reptilia au ndege pia. Mbung'o hupata vidusiwa wao kwa njia ya harufu hasa. Harufu ya wanyama wengine huvutia mbung'o na ile ya wengine huwachukiza. K.m. pundamilia na kuro hawavutii mbung'o, na hata binadamu havutii sana mbung'o wa nyika lakini anavutia mbung'o wa mito.

Spishi za mbung'o zinaweza kugawanywa katika makundi matatu: zile za nyika, zile za misitu mikuwba na zile za misitu kando kando ya mito na maziwa. Kila kundi lina vidusiwa linavyopendelea. Mbung'o wa nyika wanapendelea vidusiwa wakubwa kama vile ngiri, tandala, ndovu na ng'ombe. Wale wa mito wanapendelea vidusiwa wadogo zaidi, pamoja na mijusi kama kenge. Wale wa misitu wanapendelea pia vidusiwa wadogo na hata ndege. Binadamu ni kidusiwa wa mbung'o-mito. Mbung'o hao hutokea Afrika ya Magharibi na ya Kati hasa. Kwa hivyo ugonjwa wa malale ni nadra katika Afrika ya Mashariki na unapatikana Uganda hasa na pia magharibi mwa Kenya (Bonde la Luangwa!)na Tanzania. Hata hivyo watu wanaweza kupata ugonjwa huu kutoka mbung'o wa nyika katika sehemu nyingine za Kenya na Tanzania, k.m. pwani na mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Mbung'o hawatagi mayai lakini buu anatoka yai ndani ya mamake. Anaendelea mpaka hatua ya tatu kisha anazaliwa. Baadaye anaingia ardhini na kuwa bundo. Kila mara yai moja linakua tu.

Kutofautiana na nzi wengine

[hariri | hariri chanzo]
Proboski Sehemu za kinywa za mbung'o zimetoholewa kuwa mrija mrefu au proboski ambao umeambatwa kwenye chini ya kichwa na unaelekea mbele.
Mabawa yaliyokunjwa Wakipumzika mbung'o hukunja mabawa yao kabisa moja likiwa juu ya ingine.
Seli kwa umbo la panga Seli ya katikati ya bawa ina umbo bainifu la panga.
Arista zenye manyoya Kila kipapasio kina arista yenye manyoya yaliyo na vitawi.
  • Glossina austeni, Mbung'o-pwani
  • Glossina brevipalpis
  • Glossina caliginea
  • Glossina fusca
    • Glossina f. congolensis
    • Glossina f. fusca
  • Glossina fuscipes, Mbung'o-mito wa Kati
    • Glossina f. fuscipes
    • Glossina f. martinii
    • Glossina f. quanzensis
  • Glossina fuscipleuris
  • Glossina frezii
  • Glossina haningtoni
  • Glossina longipennis
  • Glossina medicorum
  • Glossina morsitans
  • Glossina nashi
  • Glossina nigrofusca
    • Glossina n. hopkinsi
    • Glossina n. nigrofusca
  • Glossina pallicera
    • Glossina p. newsteadi
    • Glossina p. pallicera
  • Glossina pallidipes
  • Glossina palpalis, Mbung'o-mito Magharibi
    • Glossina p. gambiensis
    • Glossina p. palpalis
  • Glossina severini
  • Glossina schwetzi
  • Glossina swynnertoni, Mbung'o Masai
  • Glossina tabaniformis
  • Glossina tachinoides