Nenda kwa yaliyomo

Fransisko Shoyemon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Kijapani ukiwaonyesha Wafiadini wa Nagasaki, karne ya 16 na ya 17.

Fransisko Shoyemon, O.P. (alifariki Nagasaki, 14 Agosti 1633) alikuwa katekista, halafu mnovisi kutoka Japani na mmojawapo kati ya Wakristo wa Kanisa Katoliki waliofia dini nchini humo.

Aliuawa na waliochukia jina la Yesu chini ya kamanda mkuu Tokugawa Yemitsu. Pamoja naye aliuawa padri mmisionari Dominiko Ibáñez de Erquicia [1].

Anaheshimiwa kama mtakatifu pamoja na Lorenzo Ruiz na wenzao waliotangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa wenye heri tarehe 18 Februari 1981 halafu watakatifu tarehe 18 Oktoba 1987.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Lorenzo de Manila, The Proto-Martyr of The Philippines and his Companions - Fr. Fidel Villarroel, O.P., 1988
  • Constantino Alvares, Jose Garcia, Pedro Tejero, Witnesses of the faith in the Orient: Dominican Martyrs of Japan, China, and Vietnam, Manila, Life Today Publications, 1989, ISBN 971-8596-03-8
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.