Nenda kwa yaliyomo

Fioretti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Fransisko na matukio ya maisha yake, 1235, Pescia, Italia.

Fioretti (kwa Kiitalia maana yake ni Maua Madogo, yaani Visimulizi Bora) ni kitabu maarufu kuhusu Fransisko wa Asizi na wenzake kilichotafsiriwa mwishoni mwa karne ya 14 kutoka kile cha Kilatini Actus beati Francisci et sociorum eius, kinachodhaniwa kuwa kiliandikwa na Ugolino Brunforte (1262 hivi – 1348 hivi).

Ingawa hakizingatiwi sana kama chanzo cha kihistoria,[1] kimekuwa na sifa kuliko vitabu vingine juu ya mtakatifu huyo, kwa uzuri mkubwa upande wa lugha na usanii katika kusimulia. Ni kama manukato yanayotuvutia kwenye roho na utakatifu wa Fransisko, aliyekwishakufa toka siku nyingi, hivi kwamba anakumbukwa kwa mbali lakini kwa namna ya kupendeza zaidi. Miaka iliyopita imechuja ujumbe wake, ambao hivyo unang’aa kwa namna ya pekee katika kitabu hicho kilichosisitiza jinsi Fransisko alivyofanana na Yesu, wazo lililokazwa na Wafransisko wote wa karne XIV.

Fioretti

Kitabu kilimuongoza Roberto Rossellini mwaka 1950 kutoa filamu Francesco, giullare di Dio (“Fransisko, Msanii wa Mungu”) akishirikiana na Federico Fellini.

Kilitumika pia kutunga libretto ya opera ya Olivier Messiaen iliyoitwa Saint-François d'Assise.

  1. Madeleine L'Engle, and W. Heywood. The Little Flowers of St. Francis of Assisi. New York: Vintage Spiritual Classic, 1998

Sehemu kubwa ya kitabu chenyewe kwa Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • Fioretti – Visimulizi Kuhusu Mtakatifu Fransisko wa Asizi – tafsiri ya Rikardo Maria, U.N.W.A. n.k. – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1996 – ISBN 9976-63-468-4

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]