Nenda kwa yaliyomo

Fasilides wa Ethiopia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Fasilides)
Fasilides wa Ethiopia


Fasilides (takriban 160318 Oktoba 1667) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kuanzia mwaka 1632 hadi kifo chake. Jina lake la kutawala lilikuwa Alam Sagad.

Alikuwa ametangazwa kuwa mfalme mkuu mwaka wa 1630 wakati wa uasi wa Sersa Krestos lakini hakuweza kuchukua madaraka mpaka baba yake, Susenyos alipojiuzulu.

Wakati wa utawala wake Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia lilipata nguvu tena. Fasilides aliwakataa wamisionari Wakatoliki.

Pia alikuwa na mabalozi mpaka Uhindi.

Aliyemfuata ni Yohannes I.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Septemba.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Uhabeshi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fasilides wa Ethiopia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.