Susenyos
Mandhari
Susenyos (takriban 1572 – 7 Septemba 1632) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kuanzia 1606 hadi muda mfupi kabla ya kifo chake alipojiuzulu. Alimfuata Za Dengel. Jina lake la kutawala lilikuwa Malak Sagad III. Susenyos alivutwa sana na imani ya kikatoliki. Aliwaalika wamisionari na hata kutangaza kuwa Mkatoliki yeye mwenyewe kuanzia mwaka wa 1622. Hata hivyo malodi wengi hawakukubali na utawala ulisumbuliwa na vita na uasi. Mwishoni Susenyos alijiuzulu na kufuatwa na mwana wake, Fasilides aliyerudisha imani ya kiorthodox.
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Uhabeshi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Susenyos kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |